Maswali ya interview (usaili) kwa kada ya ualimu Ajira Portal yapoje?

PDF Maswali ya interview (usaili) kwa kada ya ualimu Ajira Portal yapoje? 2025

Haya hapa Maswali ya interview ya ualimu (Usaili Wa Walimu) Ajira Portal katika nafasi za kazi mblimbali zilizo tangazwa na Utumishi Sekretarieti ya Ajira. Pitia haya maswali kwa umakini ujiweke katika njia sahihi.

Maswali ya interview (usaili) kwa kada ya ualimu​

1. Eleza maana ya “ELIMU”.

2. Taja sifa za mtu aliyeelimika.

3. Taja na fafanua njia kuu tatu za kupata elimu.

4. Taja na fafanua madhumuni manne ya elimu ambayo yanakidhi nchi zote duniani.

5. Chagua madhumuni matano kati ya madhumuni ya elimu Tanzania, na fafanua manufaa ya kila moja kati ya hayo.

6. Fafanua mfumo rasmi wa elimu ya Tanzania.

7. Taja na fafanua sifa tano za mfumo rasmi wa elimu.

8. Eleza maana ya mfumo wa elimu usio rasmi.

9. Eleza tofauti iliyopo kati ya mfumo rasmi na mfumo usio rasmi wa elimu.

10. Eleza maana ya madhumuni Elimu ya Jadi.

11. Taja na Fafanua sifa kuu tano za Elimu ya jadi.

12. Fafanua maarifa na stadi zilizofundishwa katika mitaala ya elimu ya Jadi.

13. Jadili mwenendo mwema na maadili yaliyokuwa katika mitaala ya elimu ya jadi.

14. “Katika Elimu ya Jadi, baadhi ya mambo waliyofundushishwa wavulana yalitofautiana na mambo waliofundishwa wasichana “Jadili usemi huo.

15. Elimu ya Jadi ilifuata mitaala gani.

16. Tanganyika(Tanzania Bara) iliwahi kutawaliwa na waarabu,eleza kwa ujumla madhumuni manne ya wakoloni hao.

17. Taja na fafanua sita tano za elimu ya shule za wamisionari.

18. Taja na jadili shabaha nne za elimu ya wajerumani.

19. Ainisha mitaala iliyotumika katika elimu wakati ukoloni wa waingereza.

20. Elimu ya wakoloni wa kiingereza ilikuwa na madhumuni gani?

21. Eleza tofauti ya mifumo ya elimu wakati wa ukoloni wa kijerumani na wakati wa ukoloni wa kiingereza.

22. Eleza kasoro tano zilizojitokeza katika elimun ya kikoloni.

23. Taja na fafanua misingi mitatu mikuu ya Elimu ya kujitegemea.

24. Elimu ya kujitegemea ilikuwa na Malengo gani?

25. Eleza mabadiliko ya mitaalayalitokona na falsafa ya elimu ya kujitegemea.

26. Eleza mambo makuu matano yaliyobuniwa na kutekelezwa chini ya mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya elimu:1969-1974

27. Taja na fafanua mambo muhimu matano yaliyoagizwa katika Azimio la Musoma.

28. “Elimu ya msingi ni elimu kamili na inayojitosheleza”.Fafanua usemi huu kwa kutoa mifano ya kutosha.

29. Eleza uhusiano uliopo kati ya azimio la Arusha na Azimio la Musoma kuhusu mambo ya kielimu.

30. Azimio la Musoma lilianisha matatizo gani ya kielimu?

31. Eleza maana na madhumuni ya Elimu ya Awali.

32. Kuna tofauti gani kati ya mitaala ya Elimu ya Awali na Elimu ya shule za msingi?

33. Eleza athari zakutumia adhabu za viboko na hasira kuwarekebisha watoto wa chekechea.

34. Mitaala ya elimu Awali imeandaliwa KIVITENDO,bali ile ya Elimu ya Msingi imeandaliwa KIMASOMO.Jadili hoja hiyo.
Maswali ya interview (usaili) kwa kada ya ualimu Ajira Portal yapoje?

Maswali ya usaili kada ya Ualimu (Walimu) - Sera ya Elimu

Maswali ya Interview kada ya Ualimu (Walimu) - Sera ya Elimu in English

Kuandaa darasa - CT 100

EA 300 notisi zote

EF 303 - Ethics
Author
GiftVerified member
Downloads
1,222
Views
5,631
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Similar resources Most view View more
Back
Top Bottom