- Views: 58K
- Replies: 7
Muktasari:
- Nafasi hizo ni za ajira kada mbalimbali huku mwisho wa kuomba ukiwa ni Februari 20, 2025
Tangazo la nafasi hizo limetolewa leo Alhamisi Februari 7, 2025 na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo.
“TAKUKURU inapenda kuajiri watumishi wenye sifa, uwezo na maadili kushika nafasi za kazi katika Idara ya Investigation officer ikiwa ni nafasi 250, Assistant investigation Officer nafasi 100.
Waombaji wanapaswa kuwa waaminifu na wasiwe na rekodi ya uhalifu. Lazima waambatishe nakala halisi na zilizoidhinishwa za vyeti vyao vya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na vyeti vya shahada/diploma ya juu, vyeti vya mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne na Sita, cheti cha kumaliza darasa la saba, vyeti vya taaluma kutoka bodi husika, pamoja na picha moja ya hivi karibuni ya pasipoti na cheti cha kuzaliwa. Aidha, ni lazima wawe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya usajili ya NIDA. Vyeti vya muda mfupi, nakala zisizo kamili, au matokeo ya mtihani hayatakubaliwa. Kwa wale walio na vyeti vya masomo kutoka nje ya nchi, ni lazima vihalalishwe na NECTA kwa elimu ya sekondari na TCU kwa elimu ya vyuo vikuu.
Waombaji pia wanapaswa kuambatisha wasifu wao wa kazi (CV) unaojumuisha anuani ya makazi inayofahamika, anwani ya posta, barua pepe, na namba za simu. Kuwasilisha vyeti vya kughushi au kutoa taarifa za uongo kwenye CV kutasababisha hatua za kisheria. Pia, wanapaswa kutoa majina ya wadhamini watatu na picha moja ya pasipoti kwa kila mmoja wao. Waombaji waliowahi kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma kwa sababu yoyote hawaruhusiwi kuomba. Barua za maombi zinapaswa kuandikwa kwa mkono kwa Kiswahili au Kiingereza. Waombaji wanaofanya kazi katika taasisi za serikali wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia waajiri wao wa sasa.
Ni wale tu watakaokidhi vigezo vilivyowekwa ndio watakaofikiriwa kwa hatua zaidi za mchakato wa ajira. Kumbuka, waombaji wote wanapaswa kufahamu kuwa watakapopata ajira, watapangiwa kufanya kazi katika ofisi yoyote ya PCCB kulingana na maamuzi ya Mkurugenzi Mkuu. Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia tovuti rasmi ya ajira ya PCCB:. Njia nyingine kama posta au kupeleka moja kwa moja hayatakubaliwa.
Bonyeza hapa ku-download tangazo
Aidha taarifa hiyo imeeleza maombi yote yafanywe kupitia mfumo maalimu wa ajira wa TAKUKURU ambao ni:
Nafasi za Kazi FAWE-Zanzibar
Ajira Mpya 2025
Nafasi za Graduate Trainee Mgodi wa Geita
Ajira Mpya 2025
Last edited: