Cassius Mailula Azigombanisha Wydad Athletic Club Na Toronto Ya Marekani

Cassius Mailula Azigombanisha Wydad Athletic Club Na Toronto Ya Marekani

Revoo

Member

Reputation: 21%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
184
Timu ya Toronto Fc ya nchini Marekani inakumbana na upinzani kutokea kwenye klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco katika jitihada za kumrejesha kikosini mchezaji wao Cassius Mailula aliyepo kwenye klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja ukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja.
FB_IMG_1736341836238.webp

Toronto wanafikiria kumrejesha kikosini mchezaji huyu kuelekea msimu mpya wa MLS mwezi Februari baada ya kuachana na kocha John Herdman ambaye hakuwa akimpatia nafasi ya kutosha kikosini, Cassius Mailula.

Mailula ambaye amewahi kuitumikia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, amekuwa na kiwango kizuri chini ya kocha Rhulani Mokwena akifanikiwa kutoa pasi 5 za usaidizi wa mabao kwenye michezo mitano ya mwisho aliyocheza. Jambo ambalo limewafanya Wydad kutanabaisha msimamo wao kuwa hawana mpango wa kumuachia nyota hiyo na badala yake wanapanga kuheshimu makubaliano baina yao kwa kusalia na mchezaji huyo hadi mwishoni mwa msimu.

Mokwena ni Baba yake katika Mpira ndio aliemfungulia njia za kuonekana katika macho ya watu, baada ya kumpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha timu ya wakubwa.
 
Back
Top Bottom