Habari Mpya Kutoka Yanga SC: Benchi la Ufundi laimarishwa

Habari za Michezo Habari Mpya Kutoka Yanga SC: Benchi la Ufundi laimarishwa

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

Gift

Administrator

Staff member
Reputation: 100%
Joined
Oct 19, 2024
Messages
1,737
Leo Young Africans SC itakuwa na matukio mawili makubwa yenye umuhimu wa kipekee kwa Wananchi. Tukio la kwanza linahusu maboresho ya benchi letu la ufundi. Habari hizi muhimu zitatangazwa kupitia Yanga SC APP, kama ilivyokubaliwa na Wananchi – taarifa yoyote isiyo kwenye Yanga SC APP haina uzito, ipotezee!

Yanga SC APP​

Katika tukio la pili, Kocha Mkuu mpya, ambaye alitangazwa rasmi jana, ameanza kazi kwa kasi ya hali ya juu. Mara baada ya kuwasili, kocha huyu raia wa Ujerumani alifanya kikao na wasaidizi wake kwa lengo la kufahamu kwa kina hali halisi ya timu. Leo, ataendelea na kikao kingine muhimu, kuhakikisha mipango na maandalizi ya kikosi yanakwenda sawia kuelekea mchezo wetu muhimu dhidi ya Al Hilal, utakaofanyika tarehe 26 Novemba 2024.
Habari Mpya Kutoka Yanga SC: Benchi la Ufundi laimarishwa

Uongozi wa Yanga SC unaonyesha dhamira ya kweli ya kuimarisha timu na kuhakikisha tunaendelea kushindana kwa mafanikio katika ngazi zote. Wananchi, ni wakati wa kusimama pamoja na timu yetu kwa nguvu zote, huku tukiamini kuwa uongozi wetu uko makini na unafanya kazi kwa ajili ya mafanikio yetu sote.

Kumbuka: Habari rasmi na za kuaminika zinapatikana kupitia Yanga SC APP. Tuendelee kuunga mkono timu yetu kwa kila hatua! 💚💛
 
Back
Top Bottom