Kuelekea Mchezo Wa Bravo Do Maquis Dhidi Ya Simba Sports Club TotalEnergies CAFCC

Kuelekea Mchezo Wa Bravo Do Maquis Dhidi Ya Simba Sports Club TotalEnergies CAFCC 2024/2025

Revoo

Member

Reputation: 21%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
190
Kuna uwezekano mkubwa Bravos do Maquis wakaingia kwenye mfumo wa Simba kama wataamini walistahili kushinda mchezo wao wa awali.

Ukweli ni kwamba Simba iliyocheza dhidi ya Bravos hapa nyumbani na hii iliyoshinda ugenini dhidi ya Sfaxien ni Simba mbili tofauti kabisa.
FB_IMG_1736501309937.webp


Nafikiri Bravos wana mechi ngumu zaidi kuliko Simba...Bravos wana presha kubwa zaidi kuliko Simba.

Kwanini...?

Simba wana sehemu ya kujiuliza kwenye mchezo wa mwisho kuliko Bravos.

Endapo Simba atapoteza dhidi ya Bravos atakuwa na mchezo mwingine nyumbani wa kujiuliza ambao kama atashinda kwa tofauti ya mabao mawili atakuwa amefuzu tayari.

Wakati huo Bravos kama atashinda mechi zote mbili atakuwa na alama 12 sawa na Cs Constantine kama atashinda mchezo ujao hivyo Head 2 Head itamuondoa Bravos kwakuwa alifungwa mabao mengi ugenini dhidi ya Constantine.

Iko hivi...

Cs Constantine akishinda dhidi ya Cs Sfaxien atakuwa na alama 12 na kimahesabu atakuwa amefuzu tayari kutokana na H2H dhidi ya Bravos na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwanini...?

Kwa sababu Simba na Bravos watakutana wao kwa wao na kama Bravos atashinda mechi zote atakuwa na alama 12 ambazo Head 2 Head inamkataa kama nilivyosema awali

Vivyo hivyo Kama Simba atashinda game zote maana yake Bravos atakuwa ameondolewa.

Salama kwa Bravos do Maquis ni kufunga mabao mengi zaidi kwasababu kama watalingana alama wote wakawa na 12 kitakachoangaliwa na H2H na ikitokea H2H ikawa na mkanganyiko idadi ya magoli kufunga na kufungwa itakuwa second option.

Namaanisha wote wakiwa na alama 12 halafu H2H kati ya Simba na Bravos ikambeba Bravos na H2H kati ya Cs Constantine na Simba ikambeba Simba wakati huo H2H kati ya Bravos na Cs Constantine inambeba Constantine unadhani kipi kitafuata? Goal difference...hapa ndipo Bravos anatakiwa kuzingatia!

Nadhani Simba hawana presha kubwa sana...wao hata wakipoteza ugenini wawekeze kwenye mchezo wa mwisho nyumbani washinde 1-0, 2-0 au 3-1 na Zaidi.
 
Back
Top Bottom