- Views: 13K
- Replies: 5
Tangazo:
- Hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TAA - Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Februari 2025 iliyo tangazwa siku ya leo tarehe 07 Februari 2025 kwa waombaji wa kada mbalimbali kuudhuria usaili/interview itakayo fanyika kama maelezo yalivyosema hapa chini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji wote wa kazi waliotuma maombi kwa nafasi mbalimbali kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 22 Februari, 2025 (usaili wa maandishi) hadi tarehe 23 Februari, 2025 (usaili wa mahojianio/ana kwa ana) katika Chuo Kishiriki cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia saa 1:00 asubuhi. Waombaji waliochaguliwa wanapaswa kufuata maelekezo yafuatayo: Kila mshiriki lazima alete kitambulisho cha utambulisho kama vile Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa/kijiji. Pia, kila mgombea anapaswa kuleta vyeti vyake halisi vya kitaaluma kama Cheti cha Kuzaliwa, vyeti vya Kidato cha Nne (Form IV) na Kidato cha Sita (Form VI), Diploma, Stashahada ya Juu, au Shahada kulingana na sifa zake.
Majina ya walioitwa kwenye usaili TAA
Ni muhimu kufahamu kuwa vyeti vya muda mfupi kama 'Testimonial', matokeo ya muda (Provisional Results), 'Statement of Results' au 'Result Slips' za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa, na wahusika hawataruhusiwa kuendelea na usaili. Aidha, kila mshiriki atajigharamia chakula, usafiri na malazi. Waombaji wanaotakiwa kushiriki usaili wanapaswa kuheshimu tarehe, muda na eneo lililotajwa bila kuchelewa. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania, ni lazima kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE, au NECTA.
Mwisho, waombaji ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili wanapaswa kuelewa kuwa hawakukidhi vigezo, lakini wanahimizwa kuomba tena nafasi zitakapotangazwa upya. Kwa wale wanaohitajika kusajiliwa na bodi maalum za kitaaluma, wanapaswa kuleta vyeti vyao vya usajili halisi.
Kuitwa kwenye interview Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
Nafasi za Kazi Jubaili Agrotech Tanzania
Ajira Mpya 2025
Nafasi za Kazi MUHAS Februari
Ajira Mpya 2025
Last edited: