Msimamo Wa Yanga Kwenye Makundi Ya CAFCL Na Nafasi Ya Kufuzu Hatua Ya Robo Fainali

Msimamo Wa Yanga Kwenye Makundi Ya CAFCL Na Nafasi Ya Kufuzu Hatua Ya Robo Fainali

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Kwenye michuano ya CAF Interclub hatua ya makundi Yanga wanaburuza mkia wakiwa na alama moja tu kwenye msimamo wa kundi A huku kinara Al Hilal akiwa na alama zake 9.
FB_IMG_1735801053587.webp


Wana nafasi ya kuongoza kundi...?

Hapa kimahesabu uwezo wa kuongoza Kundi kwa Yanga haupo tena

Kivipi...?

Yanga wamebaki na alama 9 za kuzipigania...Wana mechi mbili nyumbani na moja ugenini ambapo wakishinda zote (3) watakuwa na alama 10, hapo ili wawe juu ya Hilal watalazimika kuomba Hilal apoteze mechi zote kitu ambacho kwenye football inawezekana ila kwa performance ya Hilal sio rahisi kupoteza mechi zote hasa ukizingatia ana mechi mbili nyumbani.

Vipi kumaliza nafasi ya pili na kufuzu robo fainali...?

Hapa Inawezekana

Yanga wana mechi mbili nyumbani dhidi ya Tp Mazembe na Mc Alger ambazo wakishinda zote watakuwa na alama 7.
FB_IMG_1735404856818.webp


Changamoto kwa Yanga ni ratiba yao...

January 04 watakuwa nyumbani kucheza na Mazembe,
January 12 watakuwa ugenini kucheza na Hilal...

Kumbuka wakati Yanga wanacheza na Mazembe jumamosi, jumapili Mc Alger atasafiri kuwafuata Al Hilal.

Usisahau, Hilal alishinda Algeria na Yanga alipata sare Ugenini DR Congo

Maana yake nini?
Kama Yanga atashinda nyumbani, Hilal naye akashinda nyumbani, Yanga atakuwa na alama 4, Hilal 12, Mc Alger 4,Mazembe 2.

Mechi itakayofuata Yanga atasafiri kumfuata Ibenge Mauritania, Je Ibenge atalageza kwakuwa atakuwa amefuzu moja kwa moja?...Mimi sijui.

Nini cha kufanya...?
Mashabiki wa Yanga kitu pekee wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuipa support timu yao kwa kwenda uwanjani jumamosi kushangilia timu yao.

Wakishinda jumamosi, wanatoboa!
 
Back
Top Bottom