Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la Kwanza mpaka la Sita I – VI

Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la Kwanza mpaka la Sita I – VI

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

Gift

Administrator

Staff member
Reputation: 100%
Joined
Oct 19, 2024
Messages
1,733
Mtaala mpya ulioboreshwa wa Elimu ya Msingi Darasa I – VI umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023, maoni ya wadau yaliyokusanywa na kuchakatwa kati ya mwaka 2021 na 2022 na matokeo ya uchambuzi wa maandiko kuhusu uzoefu kutoka nchi nyingine. Mtaala huu unazingatia dira ya elimu inayolenga kumwandaa Mtanzania aliyeelimika, na mwenye maarifa, stadi na mitazamo chanya anayethamini usawa, haki na elimu bila ukomo katika kuleta maendeleo endelevu ya kitaifa na kimataifa. Vilevile, Mtaala huu umezingatia malengo makuu ya elimu pamoja na malengo ya elimu ya msingi nchini Tanzania. Kwa kuzingatia haya, Mtaala huu umeweka viwango vya utoaji wa elimu katika ngazi ya Elimu ya Msingi kwa kubainisha ujuzi, maarifa, stadi na mwelekeo atakaoujenga mwanafunzi, umahiri wa jumla, maeneo makuu ya ujifunzaji, umahiri mkuu na mahususi, njia za ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, Mtaala umebainisha muda utakaotumika katika utekelezaji, lugha ya kujifunzia na kufundishia, vifaa vya kufundishia na kujifunzia na njia zitakazotumika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa kuzingatia ujenzi wa umahiri. Hali kadhalika, Mtaala umebainisha sifa za kitaaluma na kitaalamu za mwalimu ambaye ndiye mtekelezaji mkuu wa Mtaala katika ngazi ya shule.
Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la Kwanza mpaka la Sita I – VI

Pamoja na matamko mbalimbali ya kisera na miongozo ya kitaifa, kikanda na kimataifa, Mtaala huu umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na Falsafa ya Elimu ya Kujitegemea inayosisitiza utoaji wa elimu inayomwezesha Mtanzania kujitegemea na kumudu maisha yake ya kila siku. Hivyo, utekelezaji wake utawezesha ukuaji wa mwanafunzi kimwili, kiakili, kihisia na kijamii. Ni matarajio yangu kuwa kupitia Mtaala huu, mwalimu atamwezesha mwanafunzi kujenga umahiri uliokusudiwa. Aidha, wasimamizi wote wa utekelezaji wa Mtaala na wadau wengine wa Elimu ya Msingi nchini watahakikisha kuwa elimu inayotolewa inakidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa, kikanda na kimataifa.
 

Download PDF

Back
Top Bottom