Bodi ya Chinangali BBT AMCOS Limited inatangaza nafasi ya kujitolea ya MENEJA (1) na MHASIBU (1). Tunakaribisha maombi kutoka kwa waombaji wenye sifa na walio na nia ya kujifunza na kuleta mabadiliko chanya katika chama chetu.
MAJUKUMU YA MENEJA
Meneja wa Chama atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezwaji wa shughuli za kila siku za Chama ambazo zitajumuisha: -
Kutekeleza na kuzingatia Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake, Sera ya Maendeleo ya Ushirika, Masharti haya, Kanuni na Sera mbalimbali zilizowekwa kwa ajili ya kuongoza utekelezaji wa shughuli za Chama;
Kuhakikisha mifumo ya utendaji na utoaji taarifa ipo madhubuti na inawezesha mawasiliano;
Kwa kushauriana na Wajumbe wa Bodi, kuandaa Mpango Mkakati, Mpango
Biashara, bajeti ya Mwaka na program ya utekelezaji;
Kuhakikisha malengo na shabaha za Chama zinafikiwa;
Kushughulikia masuala yote yanayowahusu watumishi, hususani mafunzo na uendelezaji wa rasilimali watu;
Kwa kushirikiana na Wajumbe wa Bodi, kuiwakilisha Chama katika shughuli na uingiaji wa mikataba;
Kuhakikisha vitabu vya hesabu vinaandikwa na hesabu zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa Wakaguzi kwa wakati;
Taarifa ya mapato na matumizi, mizania na taarifa nyinginezo zinandaliwa
kwa usahihi na wakati;
Kutoa taarifa za menejimenti kwenye vikao vya Bodi ambazo zinaeleza hali ya kifedha ya Chama ikianisha Mizania, hesabu ya Mapato na Matumizi, Bajeti ya
Mwaka, mwenendo wa Chama na uwiano wake;
Kuidhinisha matumizi yaliyoko kwenye makisio kwa viwango vilivyowekwa na Bodi na kutia saini kwenye nyaraka zinazoruhusu utoaji fedha za Chama kwa kuzingatia ukomo ulioainishwa kwenye Sera za Chama;
Kuisaidia Bodi katika kubainisha dhamana zinazokubalika na zinazoweza kutumika kudhamini mikopo;
Kuhakikisha kuwa kuna ukwasi wa kutosha kuendesha shughuli za Chama.
Kusimamia ufunguaji na uendeshwaji wa akaunti;
Kuajiri au kuwafukuza kazi watumishi, kulipa mishahara, posho na malipo mengine kama yatakavyoidhinishwa na Mkutano Mkuu, kuwatuza na kuwapandisha vyeo watumishi au kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wakosaji;
Kutoa taarifa stahiki kwa mamlaka zinazohusika kwa muda muafaka;
Kutekeleza mapendekezo yanayotolewa kwenye taarifa za wakaguzi wa ndani na wa nje na taarifa za kiuchunguzi zinazotolewa na mamlaka husika.
Kufanya kazi na majukumu mengine kadri ya maelekezo ya Bodi.
MAJUKUMU YA MHASIBU:
Kusimamia vitabu vya hesabu na kumbukumbu za kifedha za chama.
Kuandaa taarifa za kifedha na bajeti za chama.
Kutekeleza na kusimamia taratibu za malipo, mapato na makusanyo ya chama.
Kufanya ukaguzi wa ndani wa fedha na mali za ushirika na kusaidia katika maandalizi ya ukaguzi wa nje.
Kusimamia sheria, sera, kanuni na miongozo ya fedha za uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini.
Kuandaa na kuwasilisha ripoti za kifedha za kila mwezi, robo mwaka na mwaka.
Kushauri bodi na Menejimenti kuhusu masuala ya kifedha.
SIFA ZA KIELIMU ZA MENEJA
Awe na elimu angalau Stashahada (Diploma) ya fani yoyote.
Shahada ya kwanza katika fani za usimamizi, mipango, kilimobiashara, ushirika, rasilimali watu (HR) au fani zinazohusiana na masuala ya uendeshaji wa miradi zitapewa kipaumbele.
SIFA ZA KIELIMU ZA MHASIBU:
Awe na angalau Astashahada (Certificate) katika uhasibu,fedha au fani nyingine inayohusiana na masuala ya fedha kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali.
Shahada ya kwanza ya uhasibu au fani zinazohusiana na masuala ya fedha itapewa kipaumbele.
Uelewa wa mifumo ya kompyuta ya uhasibu kama vile OuickBooks, Tally, au Sage ni muhimu. Ujuzi mzuri wa Microsoft Excel na programu za ofisi ni faida.
UZOEFU:
Uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika kazi ya menejimenti na uhasibu au fedha ni faida lakini wenye hamasa kubwa ya kujifunza watapewa nafasi.
SIFA ZA JUMLA:
Uaminifu, uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu,.
Uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na timu.
Ujuzi mzuri wa mawasiliano na utatuzi wa migogoro na matatizo.
Umakini katika kufuata taratibu na uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea.
Awe ni mwanachama wa Chinangali BBT AMCOS Ltd.
FAIDA:
Nafasi hizi zitatoa fursa ya kipekee ya kujifunza na kuimarisha ujuzi katika menejimenti na uhasibu. Uzoefu wa kufanya kazi katika vyama vya ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) hapa nchini.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yaletwe moja kwa moja katika Ofisi ya Katibu yakiwa na Barua ya maombi, Wasifu (CV), na Nakala za Vyeti vya Elimu. Barua iandikwe kwa Mwenyekiti wa Bodi kupitia anuani ifuatayo:
MENYEKITI WA BODI,
CHINANGALI BBT AMCOS LTD,
S.L.P. 2182 DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Novemba, 2024 Saa 04:00 Asubuhi.
NB: “Nafasi hii ni ya kujitolea lakini itatoa fursa ya kupata uzoefu wa uhasibu na uwezekano wa kuzingatiwa kwa nafasi za kudumu katika siku zijazo”.
Kwa maelezo zaidi, tembelea ofisi yetu au wasiliana nasi kwa simu: +255 744 329 710

Attachments