TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – IDARA YA UHAMIAJI
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni Na. 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizi ni za Askari wa Uhamiaji.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji - Dodoma
Tarehe: 29 Novemba 2024
Endelea kufuata maelekezo haya kwa umakini ili kuhakikisha maombi yako yanazingatiwa.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni Na. 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizi ni za Askari wa Uhamiaji.
SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe raia wa Tanzania.
- Asiwe amewahi kuajiriwa katika Taasisi yoyote ya Serikali.
- Awe na cheti cha kuzaliwa.
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
- Awe na afya njema ya mwili na akili.
- Asiwe amewahi kutumia dawa za kulevya.
- Asiwe na kumbukumbu za makosa ya jinai.
- Asiwe na alama za michoro (tattoo) mwilini.
- Asiwe na historia ya kuolewa au kuoa na bado kuwa na mtoto.
- Elimu:
- Kidato cha Nne: Umri kati ya miaka 18-22.
- Kidato cha Sita/Stashahada: Umri kati ya miaka 18-25.
- Shahada/Stashahada ya Juu: Umri kati ya miaka 18-30.
- Awe tayari kufanya kazi mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kufuata mafunzo yote ya kijeshi na kazi za Idara ya Uhamiaji.
MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:
- Waombaji wenye Shahada, Stashahada, au Astashahada katika fani zinazotambulika na Serikali zifuatazo:
- Lugha za Kimataifa, Uhasibu, Uhasibu Mahsusi, TEHAMA, Usimamizi wa Manunuzi, Takwimu, Uchumi, Sheria, Uhandisi wa Magari, Brass Band, na Mpiga Chapa (Printer).
NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:
Maombi yote yapitie mfumo wa mtandaoni kupitia tovuti rasmi: www.immigration.go.tz kisha bonyeza kiungo hiki "Vacancies" Au Hapa pia, kupitia akaunti ya Uhamiaji ya kwenye mtandao wa Instagram hapa- Maombi yaanze tarehe 29 Novemba 2024 na kuhitimishwa tarehe 13 Desemba 2024.
- Picha ya pasipoti (passport size) ya hivi karibuni (jpg/png isiyozidi 300kb).
- Barua ya maombi.
- Barua ya Utambulisho kutoka Serikali za Mtaa/Kijiji au Shehia.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
- Vyeti vya elimu na taaluma.
- CV ya Mwombaji.
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 NECTA
- Ada na gharama za mafunzo kwa vyuo vinavyomilikiwa na VETA
- Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2025/2026
- Jinsi ya Kujiunga na Kujisajili na Showmax kwa Watumiaji wa DStv
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 NECTA Mkoa wa Dar es Salaam
TAHADHARI:
- Maombi yote yapitie mfumo wa mtandao pekee.
- Waombaji wasiofuata maelekezo watachukuliwa hatua za kisheria.
- Epuka matapeli wanaodai malipo au rushwa kusaidia maombi ya ajira.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji - Dodoma
Tarehe: 29 Novemba 2024
Endelea kufuata maelekezo haya kwa umakini ili kuhakikisha maombi yako yanazingatiwa.
Attachments
Last edited: