Nafasi za Ufadhili wa Masomo Nchini Uturuki (Turkiye Scholarships)

Nafasi za Ufadhili wa Masomo Nchini Uturuki (Turkiye Scholarships) 2025/2026

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO NCHINI UTURUKI (TÜRKIYE SCHOLARSHIPS) KWA MWAKA 2025/2026

Ubalozi unapenda kuarifu kwamba Serikali ya Uturuki imetangaza fursa za ufadhili wa masomo kupitia Mpango Maalum wa Ufadhili wa Elimu unaojulikana kama Turkiye Burslari. Ufadhili huo ni kwa ajili ya Shahada ya Kwanza, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu katika mwaka wa masomo 2025/2026.
Nafasi za Ufadhili wa Masomo Nchini Uturuki (Turkiye Scholarships)

Ufadhili huo unajumuisha ada ya masomo, posho ya kujikimu kwa mwezi, bima ya afya, tiketi ya ndege, udahili wa chuo na usajili wa kozi (University and Program Placement), makazi na gharama ya kujifunza Lugha ya Kituruki kwa mwaka mmoja (Turkish Language Course).

Taarifa zaidi kuhusu ufadhili huo ikiwa ni sifa na taratibu za uombaji zinapatikana kupitia Tovuti (https://turkiyeburslari.gov.tr). Maombi yote kuhusu ufadhili huo yatafanyika kupitia tovuti tajwa kuanzia tarehe 10 Januari 2025 na mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 20 Februari 2025.

Kwa kuzingatia umuhimu wa fursa hizi katika kuimarisha umahiri wa rasilimaliwatu nchini, Ubalozi unatoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi hizo kwa lengo la kuiletea Taifa letu maendeleo.
UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ANKARA
JANUARI 2025
 
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom