- Views: 21K
- Replies: 2
Hili hapa Tangazo la Nafasi 8000 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali VETA Januari 2025. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekelezaProgramu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifakupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadiambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbalizikijumuisha ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi,Useremala, Uchomeleaji na uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi yaalama, Upishi, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari naMitambo, umeme wa majumbani na viwandani, Umeme wa Magari, Hudumaza Hoteli na Utalii, Ukataji Madini na Ufundi vyuma.
Ofisi inapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fanizilizoorodheshwa hapo chini wafike katika vyuo vya VETA vya Mikoa na Wilayapamoja na vyuo vilivyoainishwa hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiungana mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi /mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwendachuoni na kurudi nyumbani. Mafunzo yataanza tarehe 03 Machi, 2025 nayatakua ya kutwa. Mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuokilicho katika Mkoa anaoishi.
Vituo vilivyokubalika na Serikali kutoa mafunzo hayo na fani zake vimeambatishwa.
Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 31 Januari, 2025 hadi 12 Februari, 2025 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:
i. Barua ya maombi ya mafunzo;
ii. Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;
iii. Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu ;
iv. Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na kuendelea);
v. Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji; na
vi. Picha nne za paspoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).
Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:
i. Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama;
ii. Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa magari na umeme wa jua (solar);
iii. Awe Mtanzania;
iv. Awe na umri kati ya miaka 15 – 35; na
v. Awe mwenye afya njema
Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbela katika nafasi za mafunzo haya;
Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya.
Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochanguliwa
Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)
NB: Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vyote vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo haya.

Attachments