Uchambuzi, Mechi Ya Simba vs Ken Gold Leo Tarehe 18 December 2024

Uchambuzi, Mechi Ya Simba vs Ken Gold Leo Tarehe 18 December 2024

Revoo

Member

Reputation: 18%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
160
Simba walimaliza game kipindi cha kwanza , walikuwa bora kwenye kila eneo (Wakiwa na mpira na wasipokuwa na mpira ….. Nafikiri ni wao tu kuwa na utulivu eneo la mwisho walitengeneza nafasi nyingi sana .

Kipindi cha pili , Fadlu Davids aliamua kuifunga game (Fabrice & Mzamiru Out then Kagoma na Oke In) hapo timu inacheza ikiwa chini sana , hakuna mtu wa kupandisha mashambulizi , iliwalazimu “Kibu , Awesu/ Ahoua na Budo/ Chasambi” kushuka chini kuifata mipira .

Hapo ndio uhai wa Ken Gold ukaanza kuonekana …. Simba wapo chini sana then hawaweki presha kuanzia juu …… ndio maana Ken Gold walipata nafasi nyingi nzuri za kubadili ubao wa matokeo ….. Yule Cabaye 👏 anajua boli.

Leonel Ateba “Two Goals ✅” amewapa shida safu ya ulinzi ya Ken Gold …. Awesu is a baller 👍 Fabrice “Passer 🔥” Nouma “What a performance 🔥” .
FB_IMG_1734537201179.webp


Ni total Domonance 👏 Simba wameonesha kwanini wapo Top Four na Ken Gold kwanini wanashikilia mkia ….. Simba walikuwa bora kwenye kila eneo kiwanjani (Pass sahihi , movements , runners eneo la mbele 🔥)

Nafikiri ubora wa Golikipa wa Ken Gold umepunguza idadi ya magoli ingeweza kuwa zaidi ya 2-0 …. Yule Ateba “Position yake imewapashida walinzi wa Ken gold kukabiliana nae” … Awesu Awesu 👍 Fabrice 🔥
FB_IMG_1734534391703.webp



Fadlu anafanya rotation ya kikosi na bado timu inacheza vile vile “Bravo 👏” amefanya kazi nzuri kwenye uwanja wa mazoezi .

NOTE : Nafikiri mmeona kwanini Ken Gold wapo nafasi ya 16 .
IMG-20241218-WA0042.webp
 
Back
Top Bottom