- Views: 16K
- Replies: 1
Majina ya Usaili ajira za TRA kutoka kesho
- Vituo vya Usaili TRA kwa Watakaoitwa kwenye Interview Mamlaka ya Mapato Tanzania
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe 21.03.2025 Bw. Kabengwe amesema kati ya waombaji 135,027 waliotuma maombi ya nafasi za ajira, waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wa kuandika.
Amesema kila muombaji atatumiwa taarifa ya kuitwa kwenye usaili katika barua pepe yake aliyoiambatanisha kwenye maombi ya kazi na kuwa waombaji wenye mahitaji maalum wamewekewa utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.
Bw. Kabengwe amesema usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 na Zanzibar ambayo ni
1. Dar es Salaam ambayo itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na
Pwani.
2. Zanzibar ambayo itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba
3. Arusha ambayo itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga
4. Dodoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora
5. Mtwara ambayo itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma
6. Mbeya ambayo itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa
7. Mwanza ambayo itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu
8. Kagera ambayo itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita na
9. Kigoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.
Bw. Kabengwe amebainisha kuwa waombaji wote watatendewa haki.
Usaili wa Ajira TRA 2025
Taarifa kwa Umma