Wananchi Leo Ni Gusa Achia Twende Kwao

Wananchi Leo Ni Gusa Achia Twende Kwao

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Baada ya Yanga kupata “Turning Point” yao pale Lubumbashi dhidi ya Tp Mazembe kwenye CAFCL leo wanarudi tena wakiwa nyumbani dhidi ya wababe hao hao kutoka DR Congo.
FB_IMG_1735990844194.webp

Sead Ramovic ametambulisha system mpya ya uchezaji ndani ya Yanga kwenye michezo mitatu ya hivi karibuni : shape ya 4-2-3-1 kama ilivyokuwa kwa Miguel hata Nabi lakini jinsi inavyofanya kazi ndio tofauti.

  • Yanga wakiwa na mpira hawahitaji pasi nyingi kufika kwenye nusu ya mpinzani wanacheza (Direct Football) na wachezaji wao wanafanya movements nyingi za hatari kwenda mbele : Mawings wao waingia ndani kuacha nafasi kwa FBs kufanya “Overlaps” hapo wanakuwa na idadi kubwa ya wachezaji (Create Overload) ngumu kukabiliana nao.

  • Yanga bila mpira hapa ndio uhatari wa Yanga ulipo , wanafanya pressing vizuri sana “High Pressing” na wanapora mipira mingi sana then wanakuwa haraka kwenye maamuzi (Decision) na kutengeneza mashambulizi kwa haraka sana “Turnovers” , hapo nafasi zinafunguka na idadi kubwa ya wachezaji (Muda / Abuya + Mawings , Aziz Ki + namba 9) wanakuwa na wachezaji kama watano hivi, ngumu kuwazuia.

Yanga baada ya mchezo wa Tp Mazembe kwenye CAFCL wamefanikiwa kufunga Magoli 16 huku wakiruhusu magoli mawili tu!.. kwa mda mfupi Ramovic amerudisha ule mtiririko mzuri wa Yanga kwenye ufungaji wa magoli na ile Energy imerejea.

Kila la kheri Wananchi
 
Back
Top Bottom