Ajira Mpya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania 2025

Ajira Mpya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania 2025 2025-02-13

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi na ajira mpya 2025 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Utumishi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za mwaka 2008, anatangaza nafasi za ajira ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vijana wenye sifa zifuatazo:
Ajira Mpya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania 2025

Namna ya kufanya maombi​

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kiungo cha ajira.zimamoto.go.tz mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28 Februari, 2025.

Mwombaji anapaswa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:
a) Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
b) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
c) Fomu ya uthibitisho wa sifa na jina kutoka kwa mganga wa serikali
d) Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA
e) Picha ya Pasipoti ya hivi karibuni
f) Namba ya mtihani wa Kidato cha Nne

Zingatia:
a) Nakala za vyeti zithibitishwe na Kamishna wa viapo au Hakimu
b) Barua zitakazowasilishwa kwa njia ya posta, mkono au kwa barua pepe hazitapokelewa
c) Waombaji wote waandike namba za simu kwenye barua zao za maombi
d) Mwombaji atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria

Imetolewa na:
John W. Masunga
KAMISHNA JENERALI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Author
GiftVerified member
Downloads
535
Views
6,151
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Similar resources Most view View more
Back
Top Bottom