What's new
Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi na Ajira Portal | Mkoa wa Geita

Ajira Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi na Ajira Portal | Mkoa wa Geita 01 Novemba 2024

Hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi na Ajira Portal | Mkoa wa Geita Tangazo la Matokeo ya Usaili kwa Waombaji Kazi PSRS 2024.

Kuitwa kazini utumishi na ajira portal
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawaarifu waombaji wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 02 Septemba 2024 na 13 Septemba 2024 kuwa matokeo ya usaili yamechapishwa rasmi. Matokeo haya yanajumuisha waombaji waliofaulu pamoja na wale waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali na wamepangiwa vituo vya kazi kufuatia nafasi zilizopatikana.
Pitia: Kuitwa kazini Kagera
Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi na Ajira Portal | Mkoa wa Geita

Maagizo kwa Waombaji Waliofaulu​

Waombaji wanaotakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi wanapaswa kufika na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo yao kuanzia kidato cha nne hadi ngazi ya juu. Vyeti hivi vitahakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi za ajira. Ni muhimu kwa waombaji kufuata muda uliowekwa kwenye barua hizo ili kuepuka kuchelewa.

Taarifa Muhimu kwa Waombaji​

Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika orodha hii, tafadhali tambua kuwa hawakufaulu usaili huu. Hata hivyo, mnaweza kujaribu tena nafasi nyingine zitakapotangazwa.

Soma zaidi: Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal

Kuhusu Geita: Mkoa wa Geita ulianzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 02 Machi, 2012, na kuzinduliwa tarehe 08, Novemba, 2013 na Mheshimiwa DKT Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkoa huu ulitokana na sehemu ya Mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga ambapo upande wa Magharibi na Kusini unapakana na Mkoa wa Kagera, upande wa Kusini na Kusini Mashariki unapakana na Mkoa wa Shinyanga na Mwanza kwa upande wa Kaskazini unapakana na Ziwa Victoria.
Author
Gift
Downloads
1,298
Views
1,667
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Back
Top