Orodha ya Majina ya Walimu walioitwa kazini Ajira Portal Februari 2025

PDF Orodha ya Majina ya Walimu walioitwa kazini Ajira Portal Februari 2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi.
Leo, Orodha ya Majina ya Walimu walioitwa kazini Ajira Portal Februari 2025 walioajiriwa kada za ualimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 20 Februari 2024 na 17 Januari 2025 kuwa matokeo ya waliofaulu yameorodheshwa rasmi katika tangazo hili.
Orodha ya Majina ya Walimu walioitwa kazini Ajira Portal Februari 2025


Bonyeza hapa Ku-download PDF

Orodha ya Waliofanikiwa na Hatua Zinazofuata​

Waliofaulu usaili – Majina yao yamejumuishwa pamoja na baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi – Waombaji wanapaswa kufika katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro (Masjala ya wazi) ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo, barua zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao za posta.
Kuripoti kwa Mwajiri – Waliofaulu wanapaswa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa ndani ya muda uliowekwa kwenye barua zao, wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki.

Kwa Wasiofanikiwa​

Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, wanashauriwa kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi nyingine za kazi zitakapotangazwa rasmi.

Muhimu: Utambulisho Unahitajika​

Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwasilisha kitambulisho cha utambulisho rasmi, ambacho kinaweza kuwa:
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Hati ya kusafiria (Passport)
  • Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Leseni ya Udereva
Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira au fuatilia matangazo rasmi ya ajira.

Usikose fursa yako – Hakikisha unachukua barua yako kwa wakati!
Author
GiftVerified member
Views
16,589
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Similar resources Most view View more
Back
Top Bottom