Dar es Salaam, 02 Aprili, 2025 Taarifa kwa Umma kuhusu Matokeo ya Usaili - Interview TRA Mtukumbuka kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza nafasi za kazi kuanzia tarehe 6 hadi 19 Februari, 2025. Mtakumbuka pia kwamba tarehe 21 Machi, 2025 Mamlaka ilitoa taarifa kwa umma kwamba baada ya kufunga zoezi la kupokea jumla ya maombi 135,027 yalipokelewa. Kati ya maombi hayo, maombi 112,952 yalikidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili wa kuandika.
Tarehe 23 Machi, 2025 Mamlaka ilitoa fursa ya siku mbili (24 na 25 Machi, 2025) kwa waomba kazi ambao walidhani walistahili kuitwa kwenye usaili wa kuandika ila hawakuitwa na baada ya kutolewa kwa fursa hiyo jumla ya maombi 71 yalikidhi vigezo na hivyo kufanya jumla ya maombi 113,023 kukidhi vigezo vya kufanya usaili wa kuandika.
Tunapenda kuwataarifu kuwa, katika maombi hayo, wapo waombaji walioomba nafasi zaidi ya moja, ambapo maombi 113,023 yaliyokidhi vigezo vya kufanya usaili wa kuandika yaliombwa na waomba kazi 86,314. Kati yao, waombaji waliofanya usaili wa kuandika walikuwa 78,544 ambao ni sawa na asilimia 91. Waombaji 7,770 ambao ni sawa na asilimia 9 hawakushiriki kwenye usaili kutokana na sababu mbalimbali.
Kama tulivyowataarifu hapo awali kuwa zoezi hili la usaili linafanywa na Mshauri Elekezi ambaye ni Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Mshauri huyu alipatika kupitia mchakato wa manunuzi kufuatia historia na uzoefu wake katika kuendesha masuala ya mitihani kwa weledi na uadilifu. Hivyo NBAA wanaendesha zoezi la usaili katika hatua zote mpaka waajiriwa watakapopatikana. Mamlaka ya Mapato Tanzania haihusiki na kutunga, kuratibu na kusahihisha mitihani ya usaili huo, hivyo itaendelea kubaki kama Msimamizi wa zoezi hili tu.
Kutokana na mpango kazi uliopitishwa, matokeo ya usaili wa maandishi yanatarajiwa kuwasilishwa na Mshauri Elekezi (NBAA) tarehe 23 Aprili, 2025 na yatatangazwa tarehe 25 Aprili, 2025 kupitia tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.