Ajira za Walimu Simbachawene na Mkenda Wakutana na NETO

Ajira za Walimu Simbachawene na Mkenda Wakutana na NETO Ajira Portal

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Ajira za Walimu Simbachawene na Mkenda Wakutana na Viongozi wa NETO.
Ajira za Walimu Simbachawene na Mkenda Wakutana na NETO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali itaunda timu ya wataalam itakayojuisha Wizara tano (5) ili kuchambua Makala ya “Non-Employed Teachers Organisation-NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya kijamii ili maoni yao yatumike kwa maendeleo ya taifa.

Waziri Simbachawene amesema hayo leo wakati wa kikao kilichoshirikisha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Viongozi wa NETO kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.

“Ninamuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi kuunda timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Fedha ili kuchambua makala hiyo ili tuweze kutumia mapendekezo yao kupata suluhu ya upungufu wa ajira kwa walimu” alisema Mhe. Simbachawene.

Aidha, Mhe. Simbachawene amesema Serikali ina haki ya kumsikiliza kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwa kuzingatia misingi ya 4R ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inazingatia misingi ya Falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga Upya), hivyo ujio wa viongozi na NETO na utayari wa viongozi wa Serikali kuwasikiliza viongozi hao ni jitihada madhubuti zinazosadifu uzingatiaji wa falsafa hiyo.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesisitiza kuwa utaratibu wa usaili unaleta ushindani, haki na kuondoa mwanya wa upendeleo kwa wasailiwa.

“Mapendekezo yenu ni mazuri na sisi kama Serikali tunasubiri timu iliyotajwa na Mhe. Simbachawene ifanye kazi ya kupitia na kuchambua Makala hiyo na kisha kuleta ushauri wa namna bora ya kuboresha mchakato wa ajira za walimu” alisema Mhe. Mkenda.

Vilevile, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amesema Ofisi yake iko tayari kuunda timu hiyo na itatoa taarifa ndani ya kipindi cha siku 30 hadi 45 zilizoelekezwa.
 
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom