Azam FC imechukua hatua kali dhidi ya Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe, kwa madai ya kuichafua jina la klabu hiyo. Kamwe amepigwa faini ya shilingi bilioni 10 kutokana na kauli alizotoa akidai kuwa Azam FC huzima taa za uwanja kila mshambuliaji wao, Prince Dube, anaposhika mpira na kuelekea golini kwa timu pinzani.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC, klabu hiyo ilieleza kwamba hatua ya kumfungulia Kamwe kesi ni sehemu ya juhudi za kulinda heshima ya timu na wachezaji wake. Walisema, “Hatukubali mtu yeyote kutumia nafasi yake kwa njia isiyo ya haki kueneza taarifa za uongo zinazoweza kuathiri taswira ya klabu yetu.”
Chanzo cha Utata
Kauli hiyo ilitolewa na Ally Kamwe katika muktadha wa mijadala ya mashabiki kuhusu mbinu za klabu kwenye soka la Tanzania. Hata hivyo, Azam FC imekana madai hayo na kuyaita ya uongo na yenye lengo la kudhalilisha sifa yao.Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC, klabu hiyo ilieleza kwamba hatua ya kumfungulia Kamwe kesi ni sehemu ya juhudi za kulinda heshima ya timu na wachezaji wake. Walisema, “Hatukubali mtu yeyote kutumia nafasi yake kwa njia isiyo ya haki kueneza taarifa za uongo zinazoweza kuathiri taswira ya klabu yetu.”