Caf Yaongeza Zawadi Kwa Mashindano Ya CHAN

Caf Yaongeza Zawadi Kwa Mashindano Ya CHAN 2025

Revoo

Member

Reputation: 21%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
190
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeweka wazi ongezeko kubwa la zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) ya mwaka 2025 yatakayofanyika Kenya, Tanzania, na Uganda.
FB_IMG_1736415994050.webp

Zawadi ya mshindi wa michuano hii imeongezwa kwa asilimia 75, ambapo sasa mshindi atapata dola 3.5milioni ambazo ni zaidi ya Sh8.7 bilioni.

Aidha, jumla ya zawadi kwa mashindano haya imeongezwa kwa asilimia 32, na kufikia dola 10.4 milioni ambazo ni zaidi ya 25.8 bilioni

Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, alisema: “CHAN ni mashindano muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa wachezaji wa soka wa Afrika, hasa wale walioko kwenye ligi za ndani, na itachangia pakubwa katika kuongeza ushindani wa kimataifa wa soka la Afrika na mashindano ya CAF.”

Mashindano ya CHAN 2025 yatakayoanza rasmi Februari 1, 2025, na kumalizika Februari 28, 2025, yatashirikisha nchi 17 ambazo tayari zimejihakikishia kufuzu, ikiwa ni pamoja na wenyeji Kenya, Tanzania, na Uganda, pamoja na mataifa mengine makubwa kama vile Morocco, Guinea, Senegal, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Nigeria, na mengineyo.
 
Back
Top Bottom