- Joined
- Dec 12, 2024
- Messages
- 182
Kocha mpya wa Singida Black Stars, Hamdi Miloud mwenye uraia pacha wa Algeria na Ufaransa, ambaye amerithi mikoba ya Patrick Aussems, ameeleza kuwa na mpango wa kuifanya timu hiyo kuwa tishio Ligi Kuu Bara kulingana na ubora wa wachezaji alionao.
“Tuna timu yenye vipaji vikubwa na nimejionea uwezo wao. Mchezo wa soka si kushinda tu bali ni kuhusu kutoa burudani kwa mashabiki. Lengo langu ni kuhakikisha timu yangu inacheza soka la kuvutia ambalo litawafanya mashabiki wa Singida Black Stars kujivunia timu yao.”
“Hatutakuwa na njia ya mkato katika kufanikisha malengo yetu. Kila mchezaji atahitajika kuonyesha kiwango cha juu cha ufanisi. Timu yangu itacheza soka la kushambulia, lakini pia tutakuwa na umakini mkubwa katika ulizi,”
“Nina imani kubwa na wachezaji wangu. Kila mmoja wao ana kipaji cha kipekee, tunahitaji kuwa na ushirikiano mzuri uwanjani ili tufikie malengo yetu".