Kikosi chetu cha Simba Sc kinapambana leo na CS Sfaxien – Kombe la Shirikisho Afrika
Leo saa moja usiku, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja wa Hammadi Agrebi, Tunis, kupambana na CS Sfaxien katika mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ni mechi ya ugenini yenye umuhimu mkubwa, kwani ushindi utatufanya kuiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali, huku wenyeji wao wakihitaji alama tatu kufufua matumaini yao.
“Michuano ya hatua hii huwa migumu kwa kila timu, hasa ukiwa ugenini, lakini tuna imani na maandalizi yetu. Tunalenga alama tatu muhimu,” amesema Kocha Fadlu.
“Tunatambua ugumu wa mechi hii, lakini ushindi utatupa nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali. Tumejiandaa vyema, tupo tayari kwa changamoto,” amesema Malone.
Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi kuhusu mchezo huu muhimu!
Leo saa moja usiku, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja wa Hammadi Agrebi, Tunis, kupambana na CS Sfaxien katika mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ni mechi ya ugenini yenye umuhimu mkubwa, kwani ushindi utatufanya kuiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali, huku wenyeji wao wakihitaji alama tatu kufufua matumaini yao.
Ugumu wa Mechi na Maandalizi Yetu
Kocha Mkuu, Fadlu Davids, amekiri kwamba mchezo huu utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha CS Sfaxien kinachojumuisha mchanganyiko wa wachezaji vijana na wazoefu. Aidha, kuwa ugenini ni changamoto ya ziada, lakini amesema kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kimwili na kiakili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana.“Michuano ya hatua hii huwa migumu kwa kila timu, hasa ukiwa ugenini, lakini tuna imani na maandalizi yetu. Tunalenga alama tatu muhimu,” amesema Kocha Fadlu.
Hamasa ya Wachezaji
Kwa upande wa wachezaji, nahodha wa ulinzi, Che Fondoh Malone, amesema kikosi kiko tayari kwa mapambano.“Tunatambua ugumu wa mechi hii, lakini ushindi utatupa nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali. Tumejiandaa vyema, tupo tayari kwa changamoto,” amesema Malone.
Usajili Mpya wa Elie Mpanzu
Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kwamba kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu, atacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho leo baada ya kuidhinishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Huyu ni nyongeza muhimu kwenye kikosi cha simba, na wanatarajia mchango wake katika mchezo huu mgumu.Faida za Kukosekana Mashabiki
Mechi ya leo itachezwa bila mashabiki kutokana na adhabu iliyotolewa na CAF kwa CS Sfaxien kutokana na vurugu za mashabiki wao kwenye mechi za awali. Aidha, badala ya mchezo kupigwa katika mji wa Sfax, utachezwa Tunis, hali inayowapa wapinzani changamoto ya ugenini katika ardhi yao wenyewe.Tunahitaji Mshikamano wa Mashabiki
Huku mechi ikiwa ya ugenini na yenye changamoto nyingi, mshikamano wa mashabiki wa Simba SC ni muhimu sana. Tunaomba dua na sapoti zenu kuhakikisha tunapata ushindi na kusonga mbele katika michuano hii.Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi kuhusu mchezo huu muhimu!