Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Polisi 2025

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Polisi 2025 23/04/2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Jeshi la Polisi Tanzania limetoa tangazo rasmi la kuitwa kwenye usaili kwa waombaji waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2025. Tangazo hilo linapatikana kupitia tovuti rasmi ya Polisi:
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI – Bonyeza hapa

Hatua za Kuangalia Majina Yaliyotangazwa:

1. Fungua Tangazo Kupitia Kiungo Rasmi:
Bonyeza kiungo hapo juu ili kufungua tangazo. Hii ni faili la PDF lenye kurasa kadhaa, likiorodhesha majina ya waombaji waliofanikiwa kufikia hatua ya usaili.

2. Tumia Kipengele cha "Search"
Ukifungua faili hilo kwenye simu au kompyuta:
  • Kompyuta: Bonyeza Ctrl + F na uandike jina lako.
  • Simu: Tafuta chaguo la "search" au "find in document" na uingize jina lako.
3. Angalia Taarifa Zinazokuhusu:
Kwa kila jina lililoitwa kwenye usaili, tangazo linaonyesha:
  • Tarehe halisi ya usaili kwa kila mkoa
  • Kituo cha kufanyia usaili (kituo cha polisi au shule)
  • Muda wa kufika (mara nyingi ni saa 1:00 asubuhi)
Andaa Nyaraka Muhimu:
Waombaji wote walioitwa wanapaswa kufika na nyaraka zifuatazo:
  • Cheti cha kuzaliwa (halisi na nakala)
  • Vyeti vya elimu (halisi na nakala)
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA
  • Nguo na viatu vya michezo.
Angalia hapa orodha.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Polisi 2025
 
Similar threads Most view View more
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom