What's new

Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka wa masomo 2025 | Wizara ya Elimu

Sia

Member
WARAKA WA ELIMU NA. 02 WA MWAKA 2024 KUHUSU KALENDA YA MIHULA YA MASOMO KWA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2025
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na idadi sahihi ya siku za masomo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka wa masomo 2025.

Ni muhimu kuzingatia utekelezaji wa Kalenda husika kwa ufanisi ili kuepuka changamoto ya kutokamilisha ufundishaji na ujifunzaji wa mada zote kwa wakati muafaka, hivyo kuwalimika kutoa muda wa kutosha unaohitajika na ujifunzaji unaowawezesha watoto/wanafunzi fursa ya kupumzika na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii katika familia na jamii zao.

Kalenda ya Mihula ya Masomo 2025

Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka wa masomo 2025 | Wizara ya Elimu

Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka 2025 ni kama ifuatavyo:
MIHULAKUFUNGUALIKIZO FUPIKUFUNGAIDADI YA SIKU ZA MASOMO
Muhula I06/01/202528/03/202508/04/202526/06/2025
Muhula II08/07/202529/08/202512/09/202505/12/2025
Jumla ya Siku za Masomo194
Tanbihi:
  • Siku za Masomo kwa mwaka ni 194.
  • Mashindano ya UMITASHUMTA yatafanyika tarehe 08/06/2025 hadi 21/06/2025, na UMISSETA yatafanyika tarehe 22/06/2025 hadi 04/07/2025.
  • Mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki (FEASSA) yatafanyika tarehe 17/08/2025 hadi 29/08/2025.
  1. Nawatakia utekelezaji mwema.
Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa
KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:

  • Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule Kanda na Wilaya, TANZANIA BARA.
  • Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania.
 
Back
Top