Kuelekea Mchezo Wa Leo December 28, 2024: Singida black star vs Simba sports club Nbc PL 2024/2025

Kuelekea Mchezo Wa Leo December 28, 2024: Singida black star vs Simba sports club Nbc PL 2024/2025

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Mechi ya leo kwa Simba ni moja kati ya mechi ngumu sana msimu huu,wanakutana na timu bora sana kiwanjan
IMG-20241228-WA0001.webp


Nje ya uwanja wapinzani wanaamini kwa trend ya matokeo ya Simba hivi karibuni hii mechi wanakwenda kupoteza!

Changamoto kwa Nswanzurimo ni game approach kwenye huu mchezo, akipokea maelekezo mengi akashindwa kuwaandaa wachezaji wake kimbinu anaweza kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao.

Najua, nje ya uwanja kuna ahadi na matumaini kibao ila kimbinu bado Singida Black Stars wanapaswa kuwaheshimu Simba.

Singida katika mechi 5 za mwisho licha ya kushinda mechi 3,kufungwa moja na sare moja wameruhusu mabao 6 huku wakifunga jumla ya mabao 9.

Simba kwenye michezo mitano ya ligi kuu imeshinda yote na kufunga mabao 13 huku wakifungwa mabao mawili tu waliyofungwa ugenini kwenye ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar.

Nini nataka kusema...?
Simba wanaweza kuwa wabovu kuwafungua wapinzani wanaokaa nyuma na wasiwe wabovu kushambulia nafasi zinazoachwa na timu pinzani inapoenda kushambulia.

Mfano mzuri ni kwa Azam Fc...waliingia bila tahadhari wakapoteza alama 3.
 
Back
Top Bottom