- Joined
- Dec 12, 2024
- Messages
- 190
Jumapili ya January 12, Simba wataingia katika dimba la Estadio 11 de Novembro kukipiga na Onze Bravos do Maquis kwenye mchezo wa 5 wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Katika mchezo huo Fadlu Davids nafahamu anatambua kuwa mchezo huo ndio utaamua hatima yao na matokeo yoyote yatakayopatikana yatakuwa na sura 2.
1) Simba kufuzu na kuongoza Kundi
2) Simba kuwa na nafasi ndogo ya kufuzu/kuondolewa
Kama Simba atashinda au kupata sare dhidi ya Bravos atakuwa amefuzu moja kwa moja na atahitaji ushindi dhidi ya Cs Constantine kuongoza kundi.
Kama ikitokea vinginevyo, Simba akifungwa asifungwe kwa zaidi ya tofauti ya goli moja kwani akipoteza kwa tofauti ya mabao 2+ atakuwa na nafasi ndogo ya kufuzu.
Kwanini...?
Simba alishinda 1-0 hapa Lupaso, maana yake akipoteza kwa 2-0,3-1 etc hata akishinda hapa nyumbani mchezo wa mwisho dhidi ya Cs Constantine atahitaji Bravos apoteze dhidi ya Sfaxien.
Kwa nature ya kundi lilivyo sio rahisi sana kumpa dhamana Cs Sfaxien, unahitaji roho ngumu kweli kweli.
Muhimu kwa Simba ni kuhakikisha wanapata alama kwenye mchezo wa jumapili kwasababu ndio mchezo utakaowapa ahueni zaidi kwenye kundi lao.
Na kwa namna Simba wanacheza ugenini kwenye hii michuano siwaoni Simba wakipoteza pale 11 de Novembro ingawa Bravos nao sio wanyonge wakiwa kwao kwani katika mechi 2 za nyumbani wamefunga jumla ya mabao 6 na kuruhusu mabao manne.
Uhatari wao ni uwezo wao wa kupiga mipira nje ya box na kushambulia kwa counter attacks...udhaifu wao pia ni kwenye set play, wamefungwa mabao mawili kwenye mipira ya kutenga kwa mechi zote walizocheza nyumbani.
Kila la heri Simba
Kila la heri Tanzania