TAARIFA YA KUITWA KWENYE USAILI, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anayo furaha kukujulisha kuwa umechaguliwa kwenye orodha ya walioteuliwa (SHORTLISTED) kwa nafasi uliyotuma maombi. Usaili utafanyika katika Ofisi za Kanda za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ulizochagua wakati wa maombi tarehe 5 Aprili, 2025 kwa waombaji wa ngazi ya Kidato cha Nne, na katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma, kuanzia tarehe 14 Aprili, 2025 kwa waombaji wa Taaluma Maalum (Professional Cadres).
Unatakiwa kuja na nyaraka halisi ulizotumia wakati wa kutuma maombi ya kazi, kama ifuatavyo:
Tafadhali kumbuka:
(a) Unakumbushwa kuvaa mavazi ambayo hayatazuia kukimbia.
(b) Tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato wa ajira na tarehe yako ya usaili (kwa waombaji wa Taaluma Maalum pekee).
Unatakiwa kuja na nyaraka halisi ulizotumia wakati wa kutuma maombi ya kazi, kama ifuatavyo:
- Vyeti vya kitaaluma
- Vyeti vya taaluma
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA (NIN)
- Barua ya utambulisho
- Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono
Tafadhali kumbuka:
(a) Unakumbushwa kuvaa mavazi ambayo hayatazuia kukimbia.
(b) Tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato wa ajira na tarehe yako ya usaili (kwa waombaji wa Taaluma Maalum pekee).
Nafasi 23 za Ajira Mpya SFUCHAS
31-03-2025