Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kuwataarifu Wasaailiwa waliofaulu mtihani wa mchujo na kuchaguliwa (SELECTED) kuwa, usaili wa vitendo na mahojiano (Practical and Oral Interviews) unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 02 Mei, 2025 hadi tarehe 14 Mei, 2025 na hatimaye kuwaajiri watakaofaulu usaili huo. Wasaailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
i. Kila Msaailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
ii. Wasaailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (Original) kuanzia Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Diploma, Diploma ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
iii. Wasaailiwa watakaowasilisha "Testimonials", "Provisional Results", "Statement of Results" au hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
iv. Kila msaailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
v. Kila Msaailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili kulingana na ratiba husika, muda wa kufika ni saa moja kamili asubuhi.
vi. Kwa wasaailiwa waliomaliza nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA).
vii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma, wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili na leseni za kufanya kazi (kwa wanaohusika).
viii. Msaailiwa haruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielektroniki kwenye eneo la usaili.
Ratiba ya usaili TRA:
Kwa taarifa zaidi, tembelea ofisi za TRA zilizo karibu nawe au tumia mawasiliano yafuatayo:

- Kitambulisho cha Taifa,
- Kitambulisho cha Mkazi,
- Kitambulisho cha Mpiga Kura,
- Leseni ya Udereva,
- Hati ya kusafiria au Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
ii. Wasaailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (Original) kuanzia Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Diploma, Diploma ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
iii. Wasaailiwa watakaowasilisha "Testimonials", "Provisional Results", "Statement of Results" au hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
iv. Kila msaailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
v. Kila Msaailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili kulingana na ratiba husika, muda wa kufika ni saa moja kamili asubuhi.
vi. Kwa wasaailiwa waliomaliza nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA).
vii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma, wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili na leseni za kufanya kazi (kwa wanaohusika).
viii. Msaailiwa haruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielektroniki kwenye eneo la usaili.
Ratiba ya usaili TRA:
Kwa taarifa zaidi, tembelea ofisi za TRA zilizo karibu nawe au tumia mawasiliano yafuatayo:
- Tovuti: www.tra.go.tz
- Namba za simu bila malipo: 0800 780078 au 0800750075
- WhatsApp: 0744 23 33 33
- Barua pepe: [email protected] au [email protected]
Nafasi za Kazi Shafa Agro Tanzania
28-04-2025