Kuwasilisha Malalamiko ya Matokeo ya Usaili TRA

Kuwasilisha Malalamiko ya Matokeo ya Usaili TRA 27-04-2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Kuwasilisha Malalamiko ya Matokeo ya Usaili TRA Kufuatia tangazo la matokeo ya usaili wa mchujo wa kuandika lililotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tarehe 26 Aprili, 2025, na ili kuhakikisha kuwa kila msailiwa anapata haki anayostahili, TRA inapenda kuwafahamisha wasailiwa ambao wana malalamiko au ufaunuzi wowote kuhusiana na matokeo hayo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya barua kwa Kamishna Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 28 hadi 29 Aprili, 2025 wakieleza sababu za malalamiko yao.

Barua hizo ziambatishwe na namba ya mtihani ya msailiwa.
Barua hizo zitumwe kupitia barua pepe ya [email protected] au [email protected].

Kwa waombaji waliopo Mkoa wa Dar es Salaam wanaweza kupeleka barua hizo kwenye ofisi ya TRA ya Kituo cha Huduma kwa Mlipa Kodi kilichopo Mtaa wa Samora wakati wa saa za kazi.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa na;
IDARA YA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU NA UTAWALA
Kuwasilisha Malalamiko ya Matokeo ya Usaili TRA
 
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom