G

Kwa nini walimu wa Uchumi hawana sifa za kuomba ajira masomo ya biashara? Ajira za Walimu

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Ni Kwa nini walimu wa Uchumi hawana sifa za kuomba ajira masomo ya biashara?

  • Tumetengwa

  • Vigezo sio vya mtu wa uchumi

  • Mfumo sio rafiki

  • Wafanye mabadiliko


Results are only viewable after voting.
*Habari za wakati huu na pole na majukumu ndugu, sisi ni walimu ambao bado hatuna ajira serikalini, tunaomba mtusaidie kupaza sauti kwa viongozi wa serikali na wizara husika, mwaka jana serikali ilitangaza nafasi za ajira kwa walimu kulingana na mapungufu na mahitaji ya mitaala yetu ya elimu na hadi sasa mchakato wa kuajili unaendelea, lakini ni kama walimu wa uchumi tumetengwa, ingali kwenye mtaala mpya kuna masomo ya biashara ambayo yanahitaji walimu wenye maarifa hayo ikiwemo sisi walimu wa uchumi, hivyo tunaomba serikali ituangalie na iangalie kwa kina nafasi ya walimu wa uchumi kwenye somo la biashara, kimantiki mwalimu wa uchumi ana uwezo 100% kufundisha somo la biashara, kwa maana maarifa ya somo la biashara ni maarifa yaleyale ya somo la uchumi kwa 100% kwa maana uchumi ni mama wa masomo yote ya biashara, kwa hoja hiyo tunaomba serikali iangalie upya hili jambo na itoe nafasi kwa walimu wa uchumi ili kufundisha somo la biashara, akiba ya walimu wa uchumi nchini ni kubwa na ipo tayari kubeba hilo jukumu kwa uzalendo, uweledi na maadili ya taaluma mama ya ualimu, tunaomba tena na tena mtusaidie ili serikali ituangalie na iruhusu walimu wa uchumi kuomba nafasi za kufundisha masomo ya biashara, ni matumaini yetu serikali yetu ni sikivu na ipo tayari kusikiliza maoni yetu.*
 

Download PDF

Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom