Waombaji kazi wote wa Kada ya MWALIMU DARAJA IIIA walioitwa kwenye usaili wa Mahojiano ya tarehe 21.01.2025 Mkoa wa Tabora mnajulishwa kuwa kuna mabadiliko ya mahali pa kufanyia usaili wa Mahojiano.
Usaili wa Mahojiano utafanyika Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tabora badala ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora kama ilivyooneshwa kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili la tarehe 11.01.2025.
Aidha, tarehe na muda wa usaili utabaki kama ulivyo kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu www.ajira.go.tz
Imetolewa na :Kitengo cha Mawasiliano Serikalini