Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili BOT - Benki Kuu ya Tanzania Februari 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili BOT - Benki Kuu ya Tanzania Februari 2025 Interview BOT

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi.

Muktasari:​

  • Majina ya Vijana 1106 wamechaguliwa au wameitwa kufanya usaili kama Aptitude Test Interview katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania imetangaza majina ya vijana 1106 waliochaguliwa walioitwa kufanya usaili idara hiyo kuanzia 15-02-2025 hadi 24-03-2025.

Tazama majina walioitwa kwenye interview BOT

Tangazo la kuitwa kwenye usaili huo limetolewa leo Alhamisi Februari 6, 2025 na Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki hiyo.
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili BOT - Benki Kuu ya Tanzania Februari 2025

"Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15-02-2025 hadi 24-03-2025. Wasailiwa watakaofuzu usaili huu na kwenda katika hatua zinazofuata watatakiwa kushiriki katika usaili wa vitendo au/na mahojiano kwa tarehe iliyoanishwa au kama watakavyotaarifiwa kwa wakati husika.

Tazama majina walioitwa kwenye interview BOT

Pia, Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

Usaili utafanyika kuanzia tarehe ilivyooneshwa kwenye tangazo hili, huku muda na sehemu ya usaili ikiwa imeainishwa kwa kila kada husika. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi, ambapo vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia anakotoka msailiwa. Pia, kila msailiwa anapaswa kufika na vyeti vyake halisi, ikiwemo cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine vinavyohitajika kulingana na nafasi aliyoomba.

Wasailiwa wanaojitokeza kwenye usaili hawatatakiwa kuwasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results au hati za matokeo za kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI results slips), kwani hazitakubaliwa na hawataruhusiwa kuendelea na usaili. Aidha, kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi. Ni muhimu kwa msailiwa kuzingatia tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili ili kuepuka changamoto zisizo za lazima. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania, ni sharti wawe wamehakikisha vyeti vyao vimeidhinishwa na mamlaka husika kama vile TCU, NACTVET au NECTA.

Waombaji wa kazi ambao majina yao hayajaonekana kwenye tangazo hili wanapaswa kutambua kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena nafasi zitakapotangazwa. Kwa kada zinazohitaji usajili wa bodi za kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuja na vyeti vya usajili pamoja na leseni zao za kufanyia kazi. Pia, kila msailiwa anapaswa kuingia kwenye akaunti yake na kunakili namba ya mtihani, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili. MUHIMU: Wasailiwa watakaoshindwa kuwasilisha nyaraka kamili kama zilivyoainishwa katika vipengele vya kitambulisho, vyeti vya taaluma, usajili wa bodi husika, na uidhinishwaji wa vyeti vya nje hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

Pia, Ratiba ya usaili wa mahojiano na vitendo imeambatanishwa katika tangazo hili

Tazama majina walioitwa kwenye usaili BOT
 
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom