What's new

Mambo Asiyoambiwa Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Chuoni.

Lucy Benjamin

New member
Kama mwanafunzi anayeingia chuoni, au aliyeko chuoni yapo mengi ambayo unaweza kuwa unayajua kuhusu chuo na yanafaa kuzingatiwa kwa ajili wa maendeleo mazuri kielimu. Majukumu ya mwanafunzi wa chuo yanagawanyika na kuelezeka katika makundi makuu manne ambayo wengi wanaweza kuwa wanayajua lakini hawana ufahamu wa kina kuyahusu. Ili mwanafunzi afanikiwe anahitaji kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Kusudi

2. Mkakati

3. Nidhamu

4. Motisha(motivation)

Kusudi: hili huwa ni lengo au nia ambayo mtu anayo katika kufanya jambo fulani. Ni sababu kuu inayomchochea mtu kufanya kitu. Moja ya nia ya wanafunzi wengi huwa kupata kazi nzuri ama kujiajili kutokana na elimu na ujuzi walionao utakaowapa nafasi yakujikomboa kiuchumi na kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Mwanafunzi anabidi ajitambue , afahamu ndoto zake ili aweze kufanikiwa.

Mkakati: huu ni mpango au njia iliyopangwa mapema ili kufikia lengo fulani. Mwanafunzi akilitambua kusudi lake anatengeneza ramani ambayo itakuwa kama mwongozo wa kutoka sehemu fulani na kwenda sehemu nyingine ambayo ni bora kuliko kule anakotoka.

Mwanafunzi mwenye mkakati mzuri huwa na ratiba rasmi inayomuongoza kila siku akiwa chuoni, mwanafunzi huyu akurupuki na huendeshwa na matumizi mazuri ya muda. Mikakati haiishi tu katika masomo lakini pia katika matumizi ya pesa za kujikimu ,wanafunzi wengi hujutia baada ya kuhitimu kwani pesa zao huishia katika starehe na anasa lakini mwanafunzi mzuri anaweza tumia pesa hiyo kutafuta passport,kulipia kozi fupi ili kujiendeleza n.k.

Nidhamu: ni uwezo wa kujidhibiti na kufuata sheria, kanuni au taratibu fulani.wanafunzi wengi ufurahia sana uhuru wanaoupata mara baada ya kufika chuo kutokana na umbali walionao kati yao na wazazi au walezi wao. Uhuru huu ushawishi sana mtu kujaribu vitu mbali mbali ambavyo mwanzo hakuweza kufanya kwa sababu ya uangalizi anaopata akiwa nyumbani.

Kuwa na nidhamu ni uwezo wa kuweka mipaka na kujizuia kutoka kwa tabia zisizofaa. Inaweza kuwa nidhamu binafsi kama kujiheshimu na ustaarabu,nidhamu za kijamii kama vile kushiriki katika shughuli za jamii, kufuata sheria n.k.

Mwisho, mitazamo ( Attitude): kila mtu ameumbwa na mwelekeo wa mawazo,hisia na tabia kuhusu vitu fulani ambao umtofautisha yeye na mtu mwingine. Chuo ni moja ya sehemu inayokutanisha watu wanaotokea maeneo tofauti ambapo watu hao huwa na mitazamo mingi na isiyofanana. Mtu binafsi anaweza kuwa na mtazamo wake ambao unamsaidia kuelewa, kukubaliana , na kushiriki ama kupinga kitu au jambo fulani.

Mitazamo inaweza kuwa chanya pale anapokubaliana nayo na kupenda kufanya jambo fulani kwa moyo wote na kujiamini kuwa ni jambo sahihi. Mtazamo huwa hasi pale anapoona ugumu na kukosa utayari kama jambo sio sahihi.



Lakini mitazamo hii isiwe kikwazo cha mtu kujifunza ama kushirikiana na watu wengine.

Kiujumla, ili kufurahia maisha mapya kama mwanafunzi wa chuo yakubali majukumu yaliyoko mbele yako ukiamini utayaweza, kuwa tayari kusaidia wengine na kuomba msaada pale unapoona ugumu katika jambo fulani. Mabadiliko huanza sasa na sio kesho.
 
Back
Top