What's new

Mambo Yanayochangia Utofauti wa Kufika Kileleni kwa Wanawake

Lucy Benjamin

New member
Moja ya mambo muhimu yanayohesabiwa kuwa mchango mkubwa wa uimara katika mahusiano ya kimapenzi ni uwezo wa kufika au kufikishwa kileleni. Sababu hii hupewa kipaumbele sana kiasi cha kwamba kama kutakuwa na upungufu wa kutimiza haja hiyo mahusiano mengi ufa. Watu wengi ukosa uelewa kuhusu maana nzima ya kufika kileleni , ambapo wengi huelewa ni suala linalohusiana na wanawake tu ,lakini kiuhalisia hali hii huwapata wote- jinsi ya ke na me. Hata hivyo asilimia kubwa ukumbwa na changamoto ya uelewa zaidi katika upande wa wanawake na uwezo wao kufika kileleni kutokana na sababu mbalimbali.

"Kufika kileleni “maana yake nini?

Kufika kileleni , au “ orgasm” , ni hali ya furaha na ya kimwili inayotokea wakati wa msisimko wa kingono. Hii ni hatua ya mwisho kabisa wakati wa tendo la ndoa ambapo mwili hujibu kwa njia ya nguvu ambayo hujumuishwa na hisia za furaha, kuachiliwa kwa mvutano wa misuli , na mabadiliko katika viwango vya homoni . Mtu anaweza pata hisia za kulidhika ambayo ni matokeo ya msisimko huo.

Mara nyingi ni rahisi kwa wanaume wengi kufika kileleni tofauti na wanawake. Hii inasababishwa na wanawake kuwa na mbalimbali ambazo hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Sababu hizi hufanya baadhi ya wanawake kufika kileleni haraka zaidi kuliko wengine. Sababu ziko katika makundi mawili ambayo uhusisha mambo ya kisaikolojia, kimwili na kijamii.

Makundi hayo ni kama yafuatayo:
  • Sababu za ndani (internal factors)
  • Sababu za nje( external factors)

Sababu za ndani

1.Anatomia
: wanawake wanatofautiana katika anatomia au maumbile ya uke kama vile upekee katika ukubwa na unyeti wa klitoris. Utofauti huu unaweza pelekea mwanamke kupata mda mrefu ama mfupi kufika kileleni . utofauti huo pia unaweza sababishwa uwezo wa kuhisi na kusisimka kwa uke wakati wa tendo.

2.Utofauti katika viwango vya Homoni: hali huu umtokea mwanamke wakati wa mzunguko wa hedhi ambapo wanawake wengi hukosa au hupata hamu kidogo na kusisimka ambako hufanya kuchukua mda kufika kileleni tofauti na siku nyingine ambazo aliwahi kukutana na mwenza wake.

3.Hali ya kisaikolojia: uwezo wa mwanamke kufurahia tendo unaenda sambamba na hali yake ya kiakili.iwapo mwanamke atakuwa na msongo wa mawazo , wasiwasi inaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kuburudishwa na tendo hata kufika kileleni.

4.Hisia: mwanamke huendeshwa na hisia na kama hana hisia na mtu anaeshiriki nae tendo basi hakutakuwa na uelewano mzuri kimwili. Uhusiano wa kihisia na mwenzi unaweza kuongeza furaha ya ngono na kufanya iwe rahisi kufika kileleni.

5.Hali ya afya: mwili unapokuwa dhaifu mambo mengi huenda tofauti kutokana na hisia, nguvu , akili na utayari wa mtu kuwa chini. Ambapo yote haya ushirikiana kuleta hali ya kuridhika. Hivyo magonjwa, dawa , na afya ya jumla yanaweza kuathiri kazi ya ngono.

Sababu za nje:

1.Muktadha wa uhusiano:
kama mahusiano yako katika hali ya kuvunjika ama hayana maelewano mazuri kati ya wahusika hushusha hisia ambazo humfanya mwanamke kutokuweza fika kileleni kwa mda mfupi. Baadhi ya wanawake wanapokosa imani na wenza wao hukosa hisia kabisa ama hupunguza hisia jambo linalofanya vigumu kwao kufika kileleni.

2.Mambo ya mazingira: wanawake wengi upenda kushiri tendo sehemu yenye kuridhisha, lenye faragha na faraja ambapo ikitokea hajavutiwa ama eneo husika halimpi uhuru basi uleta hofu na wasiwasi ambapo inaweza fanya ugumu wa yeye kufika keleleni tofauti sehemu yenye shwari kwake.

3. Elimu na uelewa : uelewa na ufahamu wa mwili wa mtu binafsi na majibu ya ngono yanaweza kuwapa wanawake nguvu ya kutafuta kile kinachowafaa na hvyo kuweka urahisi wakufika kileleni. Kama vile kuwa wawazi kwa wenza wao namna wanavyopenda kufanyiwa wakati wa tendo bila kusita.

Ni dhahiri kwamba sababu za wanawake kutofautiana wakati wa kufika kileleni ni nyingi na zinategemea mambo mbalimbali. Kila mwanamke ana uzoefu wa kipekee , hivyo nimuhimu kwa wanawake na wenza wao kuzungumza waziwazi kuhusu hisia zao na mahitaji yao ili kuweza kuridhishana kimwili.
 
Back
Top