Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa limeidhinisha matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi katika ngazi ya I, II na III iliyofanyika mwezi Desemba, 2024. Mitihani hiyo iliratibiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Jumla ya watahiniwa 41,331 walifanya mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi ambapo wasichana ni 14,215 sawa na asilimia 34.4 na wavulana 27,116 sawa na asilimia 65.6.
Matokeo yanapatikana kwenye tovuti ya VETA veta.go.tz
Jumla ya watahiniwa 41,331 walifanya mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi ambapo wasichana ni 14,215 sawa na asilimia 34.4 na wavulana 27,116 sawa na asilimia 65.6.
Matokeo ya Mitihani:
Kati ya watahiniwa 41,331 waliofanya mitihani, watahiniwa 35,355 sawa na asilimia 86 wamefaulu. Watahiniwa 5,976 sawa na asilimia 14 wanapaswa kurudia mitihani yao. Matokeo ya mitihani hiyo ni katika fani za Ufundi Magari, Ufundi Umeme, Ushonaji, Uchapaji, Usindikaji Vyakula, Huduma za Biashara, Kilimo, Madini, Ukarimu na Utalii pamoja na Urembo.Matokeo yanapatikana kwenye tovuti ya VETA veta.go.tz