Mchezo Umetamatika: Kagera Sugar 2 vs 5 Simbasc

Mchezo Umetamatika: Kagera Sugar 2 vs 5 Simbasc

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
🚨𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 🏆#NBCPremierLeague

Kagera Sugar 2-5 Simba Sports Club
⚽Kapombe
⚽Ahoua
⚽Ngoma
⚽Mukwala
⚽Mukwala
20241221_175648.webp

Leo ilikua mechi ya kwanza Kwa Elie Mpanzu kuitumikia Simba Hakika Anajua wanasimba wenyewe wameona....

Touch turn and shoot,touch turn and shoot yes! Ni style mpya mjini ambayo imeletwa na “mkutano wa Sadc” (Elie Mpanzu).

Kwanza yuko sharp,quick,energetic,combative halafu miguu yake ina swagger haswaa.

Leo Simba walipohitaji ku-speed Up mchezo basi mkutano wa Sadc (Elie Mpanzu) alifanya hivyo…..jamaa yuko so quick🔥

Fadlu anahitaji Fluidty na Mkutano wa Sadc umempatia hicho kitu…..jamaa anakwenda kulia,kati na kushoto.

Kilicho kosekana leo ni magoli ila hii ni shida nyingine kwa mabeki wa NBC.

Yes! The long wait is over na mkutano wa Sadc umefanyika kwa mara ya kwanza Kaitaba ndani ya dakika 57.

Karibu sana Tanzania “Mkutano wa Sadc” (Elie Mpanzu).
FB_IMG_1734793474780.webp

Kiungo Ahoua akiendelea alipoishia, Leo kaweka tena ni fundi haswa huwezi shinda bila kua na Mchezaji wa kuamua mechi ni mzuri Zaidi Kwenye kutengeneza namba.

Jean Charles ahou atawashangaza wengi msimu huu, anafanya anavyopenda yeye na sio ambavyo watu wanapenda, wachezaji wa aina hii mara nyingi wanakuwa na takwimu nzuri sana kwenye maisha yao ya soka.
20241221_165228.webp

Simba walianza mchezo vizuri : kuzuia kuanzia juu then hakuna nafasi kwenye mpira pale Kagera wakiwa na mali …. Simba walipata nafasi kubwa kwenye mpira , hakuna pressing baina ya mchezaji na mchezaji (Kagera walikuwa wazi sana) nafasi baina ya walinzi na viungo How ?

Simba wakiwa na mpira wale FBs walitanua uwanja kuiwafanya Kagera kuzuia eneo kubwa la uwanja then mawings wanashambulia nafasi finyu kati ya CBs na FBs wa Kagera Sugar hapo nafasi zikaanza kufunguka (Ahoua ni rahisi kuifikia defense ya Kagera akiwa na mpira , Mpanzu & Awesu/ Chasambi wanaongeza Options za kupasi mipira kilochobaki ni Simba watafunga magoli mangapi .

Nafikiri “Melis Medo” alikosa njia sahihi ya kukabiliana na “Offesive Transition” za Simba hasa pale wanapopoteza mipira kwenye kipindi cha kwanza , wachezaji wengi wanakuwa (Out of Position) …. Kipindi cha pili Kagera walimiliki mpira vizuri sana + Fadlu aliamua kuifunga game (Kagoma na Mzamiru In then Fernandes na Ngoma Out) Simba wakawa wanazuia kwenye “Midblock” hawapress kuanzia juu tena .

Hapo timu inakuwa chini sana Kagera wakawa na umiliki mzuri wa mchezo , nafasi zikaanza kupatikana kwa Kagera Sugar .

Jean Ahoua : Numbers kwake sio shida zake 🔥 Chasambi “3 Assist ✅” Mukwala game bora sana 🤝 Magoli mawili 🔥 …… Ellie Mpanzu kacheza vizuri kwa dakika alizokuwa uwanjani . No Cleansheet kwa Camara .

FT : Kagera Sugar 2-5 Simba Sc .
FB_IMG_1734545632228.webp

Ladack Juma Chasambi jezi namba 36 mgongoni kutoka Kisaki Morogoro, Ndui bega la kulia na miaka 19 tangu alione jua

Leo dhidi ya Kagera Sugar amehusika kwenye mabao 3 kati ya matano ya Mnyama Simba

Assist moja kwa Fabrice Ngoma na Assist mbili kwa Desse Mukwala

Top Perfomance 🔥
FB_IMG_1734793321196.webp
 
Back
Top Bottom