Mchezo Umetamatika: Yanga 5 vs 0 Fountain Gate Nbc PL 2024/2025

Mchezo Umetamatika: Yanga 5 vs 0 Fountain Gate Nbc PL 2024/2025

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Yanga walianza na mikakati sahihi , wakiwa na mpira 2-3-4-1 (Joba na Bacca wanakuwa nyuma then Aucho mbele yao “Pembe tatu shape” huku Kibwana na Boka wanakuwa mstari mmoja then Muda anasogea juu sawa na Aziz Ki , Pacome na Mzize …. Baada ya hapo matokeo yake yalikuwa ni nini ?

Yanga walifanya pressing vizuri sana bila mpira : Muda , Aziz Ki , Pacome na Mzize walipora mipira mingi hasa Fountain wanapoanza “Build Up” yao …. Magoli matatu ya Yanga yametokana na “Quicky Transitions” pale wanapopora mipira wanaunda mashambulizi kwa uharaka sana (Yanga walipata runners wengi eneo la mbele , movements sahihi na maamuzi sahihi ) .
FB_IMG_1735484978624.webp

Fountain Gate plan yao ni kuanza “Build Up” kuanzia chini tena kwa pasi fupi fupi lakini idadi ya wachezaji wao wakati wanafanya progression ilikuwa ndogo Vs idadi ya wachezaji wa Yanga + pressing ngumu kwa Fountain Gate kuishinda pressing ya Yanga .

Baada ya kubadilika kwenye plan yao wakawa wanatumia mipira mirefu kushambulia (Edger , Ambundo na Kihimbwa) , lakini Yanga walihakikisha wanashinda mipira yote ya juu na second balls zote …. Kwasababu hawakuacha nafasi kubwa kati ya kiungo na walinzi (Job na Bacca) hawakuzuia wakiwa chini sana .

Ile Pressing ya Yanga imeanza kurejea (wanapress vizuri sana (Muda , Aziz , Pacome na Mzize nyuma ya Dube) hapo wanakuwa na wachezaji wengi kwenye nusu ya FG

Magoli matatu kati ya matano ya Yanga yametokana na “Quickly Transition” wakipora mipira wanakuwa na idadi kubwa ya wachezaji + runners wengi eneo la mbele …. Muda “Energetic ✅” Mzize “Two Assists 🔥” .

NOTE :

Magoli matatu ya Yanga yote yametokana na “Quicky Transition” wakipora mipira wanakuwa haraka kwenye maamuzi yao .

Pacome ✅ Mudathir timu isipokuwa na mpira “Energetic 🔥” anazuia eneo kubwa la uwanja + runners mzuri 👍

Job na Bacca✅ Kibwana kaubonda sana 👍 Aucho kwenye kiungo 🔥

Clement Mzize “Two Assists & One Goal” kacheza game bora ✅

FT : Yanga 5-0 Fountain Gate .
20241229_180619.webp
 
Back
Top Bottom