Mfumo wa Anwani za Makazi NAPA Tanzania

Mfumo wa Anwani za Makazi NAPA Tanzania Mawasiliano

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 48%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
411
NaPA ni mfumo wa kidigitali wenye kanzidata ya anwani za makazi. Kupitia mfumo huu mwanchani anaweza kupata huduma zilizopo karibu kama hospitali, ATM, Benki na n,k, anaweza kupata uelekeo kutoka anwani moja hadi nyingine na kupata postikodi ya maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, inatekeleza Mfumo wa Kidigitali wa Anwani za Makazi na Postikodi. Lengo la utekelezaji wa Mfumo huu ni kuhakisha kila taasisi ama mwananchi anakuwa na Anwani ya Makazi katika eneo lake la nyumbani, ofisini ama biashara.

Faida za matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi
  • Kurahisisha utoaji, upatikanaji na upelekeaji wa huduma na bidhaa kwa wanachi/wateja;
  • Inawezesha biashara mtandao na upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii kama vile za afya;
  • Kutambua eneo kirahisi na kufahamu mahali alipo mtu au kitu hivyo kupunguza muda na gharama za usafiri;
  • Inaongeza kasi ya kupambana na uhalifu, kuimarisha shughuli za uhamiaji, utalii, ulinzi na usalama.
  • Kurahisisha upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za maendeleo ya kibiashara na kijamii.
  • Inaongeza tija kwenye huduma za uokoaji na maafa;
Napa itakuwezesha;
1. Kujua anuani yako: Fahamu Anwani unayoishi na Anwani ya Taasisi
2. Tafuta Postikodi: Fahamu Postikodi ya eneo lako unaloishi
3. Tafuta Address Kodi: Fahamu Addresskodi ya eneo unaloishi
4. Barua ya Utambulisho: Pata Barua ya utambulisho wa ukaazi.

Soma zaidi kuhusu Napa hapa
Mfumo wa Anwani za Makazi NAPA Tanzania
 
Similar threads Most view View more
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom