MO DEWJI, AKABIDHIWA REPORT KAMILI YA USAJIRI MSIMBAZI

MO DEWJI, AKABIDHIWA REPORT KAMILI YA USAJIRI MSIMBAZI

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Baada ya kuwasili nchini mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi ya Simba SC, Mohammed Dewji 'Mo' amekabidhiwa ripoti ya usajili ya dirisha dogo ya klabu ya Simba SC kutoka kwa bechi la ufundi la Simba linaloongozwa na kocha mkuu Fadlu Davids.

Katika ripoti hiyo kocha Fadlu anahitaji wachezaji watatu hadi wanne, beki wa kati, Kiungo mshambuliaji, winga na mshambuliaji katika ripoti hiyo Fadlu anataka beki mwingine wa kati mzawa mwenye uwezo kama Hamza, pia anataka kiungo mshambuliaji ambaye ataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

Nafasi ya winga atachukua Ellie Mpanzu ambaye anasubili dirisha la usajili lifunguliwe ili aweze kuingizwa kwenye mfumo kuchukua nafasi ya golikipa Ayoub Likred ambaye ameshamalizana na Simba na ataondolewa kwenye usajili huku akihitaji mshambuliaji mwingine mzawa au wa nje mwenye uwezo.

Pia katika mapendezo hayo Fadlu ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumuongezea mkataba mpya kiungo Fabrice Ngoma ambaye kwa sasa amekuwa anafanya vizuri huku winga Joshua Mutale raia wa Zambia anaweza kuondolewa kwenye mfumo wa usajili ili kusajiliwa mchezaji mwingine wa kimataifa kutokana na kuwa na majereha ya mara kwa mara.

Wachezaji wengine 10 wa kimataifa wenye uhakika wa kubaki ndani ya klabu ya Simba ni golikipa (1) Mussa Camara, Mabeki (3) Valentine Nouma, Chamou Karaboue, Che Malone, Viungo (4) Augustine Okejepha, Deborah Fernandez, Fabrice Ngoma, Charles Ahoau, Washambuliaji (2) Steven Mkwala na Lionel Ateba.
 

Attachments

  • FB_IMG_1733919639423.webp
    FB_IMG_1733919639423.webp
    40.7 KB · Views: 42
  • FB_IMG_1734160486928.webp
    FB_IMG_1734160486928.webp
    47.9 KB · Views: 30
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom