Muda wa Uhamisho Cheti na Diploma Waongezwa NACTVET

Muda wa Uhamisho Cheti na Diploma Waongezwa NACTVET 26-04-2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 54%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
453
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautangazia umma kuwa zoezi la uhamisho wa wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa ngazi ya Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) limeongezwa muda hadi tarehe 1 Mei, 2025.
Muda wa Uhamisho Cheti na Diploma Waongezwa NACTVET

Baraza linawasisitiza wanafunzi kuwasilisha maombi yao mapema kwa kuzingatia masharti na vigezo vya uhamisho vilivyowekwa ili kuepuka usumbufu.

Aidha,vyuo vinakumbushwa kutimiza wajibu wao kwa kushughulikia maombi yote ya uhamisho yatakayowasilishwa kabla ya tarehe 30 Aprili, 2025 na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa
 
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom