Mzamiru Afunguka Kuelekea Mchezo Wa Kesho Jumapili 05 January 2025.

Mzamiru Afunguka Kuelekea Mchezo Wa Kesho Jumapili 05 January 2025.

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
KIUNGO wa Simba Mzamiru Yassin amesema mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) dhidi ya Sfaxien ya Tunisia haitakuwa nyepesi wanahitaji jitihada, umakini na nguvu kuhakikisha wanapata matokeo.
FB_IMG_1735972450242.webp

“Mechi za ugenini huwa ni ngumu haijalishi umecheza na timu gani tunatakiwa tuwe makini, mtu anapopata dakika za kucheza ajitoe kwa kuonesha jitihada za hali ya juu kuisaidia timu.

“Wapinzani wetu hawajapata matokeo sio kwamba ni wabaya bado tunapaswa kuwaheshimu, ni mechi ngumu inayohitaji umakini, kwa jitihada zetu na nguvu zetu tunaweza kupata ushindi,”amesema Mzamiru.

Wekundu hao wa Msimbazi wako kundi A wakishika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo mitatu na kati ya hiyo, kushinda miwili, kupoteza mmoja wakiwa na pointi sita sawa na kinara Bravos ya Angola na CS Constatine ya Algeria nafasi ya pili kukiwa na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.
 
Back
Top Bottom