G

Nafasi 20 za kazi Assistant Customer Service Officer II TAA November 2024

GiftVerified member

Administrator

Staff member
Reputation: 94%
Joined
Oct 19, 2024
Messages
665
Kwa niaba ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inakaribisha Watanzania wenye sifa na uwezo unaohitajika kuomba nafasi kumi (10) za kazi zilizotajwa hapa chini.

NAFASI: MSAIDIZI WA HUDUMA KWA WATEJA DARAJA LA II – NAFASI 10
MWAJIRI:
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
MUDA WA MAOMBI: 29 Novemba 2024 hadi 12 Desemba 2024

Majukumu ya kazi:

  1. Kutambua wateja na mahitaji yao.
  2. Kuwasiliana na wateja wa uwanja wa ndege na kuwapa taarifa na mwongozo kuhusu masuala yanayohusu huduma zinazotolewa.
  3. Kushirikiana na idara nyingine kuhusu masuala ya huduma kwa wateja na kutoa ripoti za kila siku, wiki, mwezi, na mwaka.
  4. Kutoa huduma bora kwa wateja kwa kuzingatia maadili ya kitaalamu katika mazingira ya kazi.
  5. Kuwasiliana na wateja kwa heshima kwa njia ya simu, barua pepe, maandishi, au ana kwa ana.
  6. Kupokea na kusambaza taarifa za mashirika ya ndege na ratiba za safari kwa abiria na wateja.
  7. Kupokea taarifa za safari kutoka kwa Watawala wa Ndege na waendeshaji wa mashirika ya ndege na kuzifikisha kwa wasimamizi na watumiaji wengine.
  8. Kutoa vibali vya kuingia (gate pass) kwa wageni.
  9. Kuhifadhi kumbukumbu za wageni wa uwanja wa ndege.
  10. Kutoa taarifa kuhusu huduma za watalii, mawakala wa usafiri, na hoteli kwa wateja.
  11. Kuongoza na kutoa maelezo kwa wageni wa uwanja wa ndege.
  12. Kufanya kazi nyingine yoyote kama atakavyoelekeza msimamizi.

Sifa za mwombaji:

Awe na Stashahada (Diploma) katika fani ya Huduma kwa Wateja, Utawala wa Biashara (maalumu katika Masoko), Biashara, Masoko, Mawasiliano ya Umma, Mahusiano ya Kimataifa, Sosholojia, au sifa nyingine zinazolingana kutoka katika taasisi inayotambulika.

Bonyeza hapa kutuma maombi
 
Back
Top Bottom