PSRS: Leo tarehe 25/10/2024 wametangaza nafasi za kazi katika ajira mpya Kwa niaba ya Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT) na Wakala wa Ndege za Serikali ya Tanzania (TGFA), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawaalika Watanzania wenye sifa, ujuzi, na uzoefu wa kutosha kujitokeza kuomba nafasi saba (7) za kazi zilizoainishwa hapa chini.
Nafasi zilizo tangazwa - 5
Nafasi zilizo tangazwa - 2
Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT)
Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT) ilianzishwa kwa Sheria ya Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji, Na. 24 ya mwaka 1982 kifungu cha 187, Toleo lililorekebishwa la mwaka 2009, kama Taasisi ya Kujitegemea ya Elimu ya Juu. Taasisi hii imesajiliwa rasmi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ikiwa na Namba ya Usajili REG/EOS/009 ya mwaka 2002.Nafasi zilizo tangazwa - 5
Wakala wa Ndege za Serikali ya Tanzania (TGFA)
Wakala wa Ndege za Serikali ya Tanzania (TGFA) ulianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 (kama ilivyorekebishwa) na kuanza rasmi tarehe 17 Mei, 2002 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 193 lililochapishwa siku hiyo hiyo. TGFA ilichukua majukumu ya Kitengo cha Ndege cha Serikali kilichokuwa chini ya Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji (sasa ni Wizara ya Ujenzi na Usafirishaji) kwa lengo la kutoa huduma za usafiri wa anga kwa Serikali kwa ufanisi zaidi, gharama nafuu, na kwa mtazamo wa kibiashara. Wakala huu ulipitishwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano hadi Ofisi ya Rais, Ikulu kupitia Tangazo la Serikali Na. 252 la mwaka 2018.Nafasi zilizo tangazwa - 2