Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, inatangaza nafasi za kazi za kujitolea kwa Kada mbalimbali kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) kama ifuatavyo:-
Maombi yatumwe kwa:-
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
S.L.P.110
MOROGORO
No | Kada | Idadi |
---|---|---|
1 | Afisa Muuguzi Msaidizi | 18 |
2 | Afisa Tehama | 1 |
3 | Mapokezi | 4 |
4 | Wapaguzi | 4 |
5 | Wahudumu wa chumba cha maiti | 2 |
6 | Mpiga picha | 1 |
7 | Radiographer | 5 |
Jumla | 35 |
Sifa za jumla kwa Kada za Afya
Waombaji wanatakiwa kuwa na:-- Cheti cha taaluma cha kada aliyosomea cha chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe amesajiliwa na Baraza la Kitaaluma kwa Kada za Afya.
- Awe na Leseni ya taaluma husika.
- Awe na cheti cha kidato cha nne/sita kinachotambuliwa na NECTA.
Sifa za jumla kwa Kada zisizo za Afya
Waombaji wanatakiwa kuwa na:-- Cheti cha taaluma cha kozi aliyosomea cha chuo kinachotambuliwa na Serikali
- Awe anajua Kiswahili na Kiingereza.
Masharti ya Jumla ya Waombaji
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:-- Awe raia wa Tanzania
- Awe na umri usiozidi miaka 45
- Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyo soma (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na Usajili kamili) “Full Registration” au Leseni inayohitajika kwa kazi ya taaluma husika
- Mwombaji awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela
- Mwombaji yaambatanishe na barua ya maombi
- Mwombaji yaambatanishe na nakala za vyeti vya Elimu, Taaluma na cheti cha kuzaliwa
- Testimonials results slip HAITAKUBALIWA
Maombi yatumwe kwa:-
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
S.L.P.110
MOROGORO