Nafasi za kazi Nguruka Development Agency (NDA) | Ajira Mpya 50 Kufanya kazi Nje ya Nchi

Nafasi za kazi Nguruka Development Agency (NDA) | Ajira Mpya 50 Kufanya kazi Nje ya Nchi

GiftVerified member

Administrator

Staff member
Reputation: 88%
Joined
Oct 19, 2024
Messages
613
Taasisi ya NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY (NDA), ni taasisi iliyosajiliwa kwa usajili namba OONGO/00004986, yenye makao makuu mkoani Kigoma na tawi jijini Dar es Salaam. Taasisi ya NDA, inajihusisha na shughuli za kimaendeleo, Mazingira na ulinzi wa haki za binadamu. NDA inatekeleza miradi yake kwa kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuchochea maendeleo ya jamii ya Kitanzania na Taifa kwa ujumla.

Hali ya Ajira Tanzania:
Hadi 2020/2021, kufuatia taarifa ya ofisi ya Takwimu Tanzania, ukosefu wa ajira Tanzania ni takriban watu milioni 2.47 wenye umri kati ya miaka 15 na kuendelea. Kati ya watu hao, milioni 2.32 wako Tanzania Bara na 150,000 Zanzibar. Takwimu pia zinaonyesha watu wengi wasio na ajira wapo vijijini ikilinganishwa na mijini kwa Tanzania Bara, na kidogo zaidi mijini kuliko vijijini kwa upande wa Zanzibar. Inaelezwa kuwa vijana wengi wasio na ajira ni vijana kati ya miaka 15-24 na 25-35.

Jitihada za kitaifa zimefanyika na kupelekea kwa ujumla ukosefu wa ajira kupungua kutoka asilimia 10.5 mwaka 2014 hadi asilimia 9.3 mwaka 2020/21. Kupungua huko pia kwa Tanzania Bara ni kutoka asilimia 10.3 mwaka 2014 hadi asilimia 9.0 mwaka 2020/21. Hata hivyo, ukosefu wa ajira Zanzibar umeongezeka hadi asilimia 19.7 mwaka 2020/21 kutoka asilimia 17.4 mwaka 2014.

Fursa kwa Vijana:
Taasisi ya NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY (NDA) katika mpango wake wa kuwezesha vijana kupata fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi na kushiriki katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini Tanzania, tunatangaza Shindano la usajili wa vijana watakao wekewa kwenye database ya taasisi kwa lengo la kuunganishiwa na fursa mbalimbali za nje ya nchi sawa na zinazopokelewa na taasisi hii.

Kwa awamu hii ya kwanza, taasisi inahitaji vijana wenye sifa zifuatazo:
  • Awe Mtanzania mwenye akili timamu.
  • Awe kijana wa kiume.
  • Awe na elimu ya kuanzia sekondari na kuendelea (Diploma ni vyema zaidi).
  • Awe na umri kati ya miaka 20-40.
  • Awe na uwezo wa kuongea na kusoma vizuri lugha ya Kiingereza.
Nafasi za kazi Nguruka Development Agency (NDA) Ajira Mpya 50 Kufanya kazi Nje ya Nchi.webp

Ajira Mpya Nguruka Development Agency (NDA)

Jinsi ya kutuma maombi:

Hatua ya kwanza:
Tuma nakala zifuatavyo kwenye email: ndatanzania@hotmail.com Cc manager@vegrab.co.tz
1. Cheti cha Elimu yako (Sekondari/Chuo)
2. Kitambulisho cha NIDA
3. Cheti cha kuzaliwa
B. Hatua ya pili:


Mara baada ya kutuma maombi, tuma pia mchongo (video) fupi (dakika moja), ukieleza kwa kifupi utu wako na uwezo wako kwa lugha ya Kiingereza.
Picha mchongo (Video) tuma katika WhatsApp number +255 769 058 814.

Gharama zote za programu hii, ikiwemo usafiri na Ndege, Malazi, Chakula, Bima ya Afya na Usafiri wa ndani hutelewa na Wadhamini wa programu hii.

Tuma maombi yako kabla ya 07/12/2024.

NOTE: HAKUNA MALIPO YA USAILI, BAADA YA USAILI, WATAKAO CHAGULIWA TARATIBU ZOTE ZA KISHERIA ZITAFIATWA IKIWEMO KUONDOKA NCHINI IKIWEMO, PASSPORT, VISA PAMOJA NA USHIRIKISHWAJI WA BALOZI NA WIZARA HUSIKA.
 
Back
Top Bottom