Nafasi za Kazi Nono Supermarket Tanzania

Nafasi za Kazi Nono Supermarket Tanzania

Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
NB: HATUJIHUSISHI NA VITU VINGINE ISIPOKUWA AJIRA.
Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 90%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
803
Hizi hapa Nafasi za Kazi Nono Supermarket Tanzania zilizo tangazwa siku ya leo kwa watanzania wote wenye nia, ari na sifa, waweze kutuma maombi.

1. Wahudumu (Supermarket Assistant)
Majukumu:
  • Kusindikiza wateja
  • Kumsaidia mteja kupata bidhaa kwa urahisi
  • Kuhakikisha bidhaa zilizopngua zinafika kwa wakati
  • Kubaini bidhaa zilizopungua
  • Kupanga bidhaa
  • Majukumu mengine yatakayo jitokeza muda wa kazi
Sifa za mwombaji:
  • Elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea
  • Umri 20 na kuendelea
  • Uzoefu usiopungua mwaka 1
  • Asiwe na rekodi ya uharifu au makosa ya jinai
  • Awe Msafi na mwenye muonekano mzuri
2. Store keeper
Majukumu:
  • Kuhakikisha idadi ya bidhaa zinazo toka na kuingia ipo sawa
  • Kutunza bidhaa kwa uangalifu mkubwa
  • Kuhakikisha bidhaa zote zina rekodiwa katika file husika
  • Kuhakikisha hakuna upungufu wa bidhaa store
Sifa za mwombaji:
  • Elimu Certificate au Diploma kwa fani yoyote
  • Awe mbobevu katika kutumia vifaa vya tehama (Compture)
  • Awe na ujuzi mkubwa wa utambuzi wa bidhaa
  • Umri 20 na kuendelea
  • Uzoefu usiopungua miaka 2
  • Asiwe na rekodi ya uharifu au makosa ya jinai
3. Mapokezi (receptionist)
Majukumu:
  • Kufanya kazi zote za Cashier
  • Kuhakikisha wateja wote wanalipa
  • Kukagua miamala yote itakayofanywa kwa njia ya Simu au Bank
Sifa za mwomaji:
  • Elimu Kidato cha nne, kidato cha sita, certificate/Diploma/degree yoyote
  • Awe na ujuzi wa kutumia compture
  • Umri miaka 20 na kuendelea
  • Awe na uwezo wa kuhudumia wateja wengi kwa muda mfupi
  • Asiwe na rekodi ya uharifu au makosa ya jinai
Jinsi ya kutuma maombi:
Mwombaji atume wasifu wake (CV), na Barua ya maombi ikionesha nafasi na Mkoa.

Cv na Barua Ziambatanishwe katika PDF moja

Maombi yote yatumwe kwa njia ya barua pepe (Email) kabla ya tarehe 20/11/2024

Marketing Manager

P.O.BOX 256

Lumumba Rd, Mwanza [email protected]
Nafasi za Kazi Nono Supermarket Tanzania

Ajira Mpya Nono Supermaket
 
Back
Top Bottom