Moja ya hatua za mwanzo kabisa za mwanafunzi katika kipengele cha elimu ya msingi ni pale anapoweza kufanya vizuri na kufaulu mitihani ya darasa la nne. Mitihani hii ufanyika kila mwezi wa kumi wa kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu mitihani hii ilifanyika tarehe 23 na 24 Octoba.Kama mzazi , analojukumu la kufuatilia na kuwa na ufahamu wa maendeleo ya mtoto sio tu kabla ya mtihani na wakati mtoto akiwa anaendelea na mtihani bali uendelea hata baada ya kumaliza mtihani.
Ufahamu ujumuisha tarehe ya kuanza mtihani na kumaliza, tarehe ya kutolewa kwa matokeo ya darasa la nne,na jinsi ya kupata taarifa sahihi kuhusu matokeo.
Kama mzazi utawezaje kuangalia matokeo ya mwanao pale unapopata taarifa kuwa yametoka?
Zifuatazo ni baadhi ya njia rahisi ambazo mzazi ama mlezi anaweza kutumia kupata taarifa kuhusu ufaulu na matokeo ya mwanafunzi ;
Kuangalia matokeo kupitia njia ya mtandao kunahitaji umakini katika kufuatilia maelekezo ya mfumo husika na pia mtumiaji anahitaji intaneti imara kuzuia matatizo wakati anaangalia matokeo.
Njia ya pili na ambayo ni rahisi, mzazi anaweza kufika shuleni kwa mwanafunzi ili kupata matokeo.
Kwa kawaida matokeo ya darasa la nne nchini hutumwa mashuleni. Baada ya Baraza la mitihani la Taifa (NECTA) kukamilisha kuchambua na kutangaza matokeo, nakala za matokeo hupelekwa shule husika.
Njia hii urahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wazazi wasio na uwezo wakupata taarifa husika kupitia mitandao , na pia nakala ya matokeo kutoka shuleni inachukuliwa kama uthibitisho rasmi wa utendaji wa mwanafunzi.
Utayari wa mzazi ama mlezi kufuatilia matokeo kwa wakati na kwa njia sahihi kunasaidia kujua maendeleo ya mwanafunzi na kujua eneo analohitaji msaada kielimu,kufanya maamuzi sahihi kuhusu masomo ya mwanafunzi katika ngazi inayofuata. Hivyo humsaidia mzazi kujiandaa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mafanikio ya mwanae.

- Kupitia mtandao: mzazi anabidi ajue taasisi ambayo inahusika na masuala ya mitihani ya kitaifa,ambapo nchini Tanzania, NECTA hutoa tovuti rasmi ambapo matokeo yanaweza kuangaliwa moja kwa moja pale yanapotoka. Lakini pia mitandaoni kunaweza kuwa na tovuti mbali mbali ama portal za elimu zenye kutoa huduma sawa na hii. jinsi ya kufanya:
- Ingia kwenye tovuti husika.
- Tafuta sehemu iliyoandikwa “Angalia Matokeo” au “Results”.
- Ingiza namba ya mtihani na tarehe ya kuzaliwa kwa mwanafunzi.
- Bonyeza “Tuma” au “Submit” kisha itakuonyesha matokeo ya mwanafunzi husika.