Hii hapa Orodha ya Majina ya Walioitwa kazini Geita Ajira za ICAP December 2024. Katibu Tawala Mkoa wa Geita anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi mbalimbali za kazi waliofanya usaili tarehe 03 Disemba 2024 kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa kwenye tangazo hili.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Geita.
Maelekezo kwa Waombaji Waliofaulu:
Waombaji waliofanikiwa na kupangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kufanya yafuatayo:- Kuripoti kazini tarehe 10 Disemba 2024 kwa mwajiri wakiwa na:
- Vyeti halisi vya masomo na taaluma, kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
- Hii ni kwa ajili ya uhakiki wa vyeti kabla ya kupokea mikataba ya ajira.
- Kumbuka:
- Mtumishi ambaye hataripoti hadi tarehe 13 Disemba 2024, nafasi yake itachukuliwa na mwingine mwenye sifa.
Kwa Waombaji Ambao Majina Yao Hayapo:
Ikiwa jina lako halimo katika tangazo hili, tafadhali elewa kuwa hukufaulu usaili. Hata hivyo, usikate tamaa; endelea kuomba nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Geita.
Attachments